BEYONCE NA JAY Z WAAJIRI WAFANYAKAZI 6 KUWAHUDUMIA MAPACHA WAO

Beyonce na Jay Z walipata mapacha hao, Rumi na Sir katikati ya mwezi Juni mwaka huu na tayari wameshaajiri wafanyakazi lukuki wa kuwahudumia nyumbani kwao jijini Los Angeles. Kwa mujibu wa jarida la OK! la nchini Marekani, wanamuziki hao wameajiri wafanyakazi 6 kwa ajili ya kuwahudumia mapacha hao ambao kila mmoja atakuwa analipwa mshahara wa dola za Marekani 100,000 kwa mwaka (zaidi ya milioni 223 kwa mwaka) zaidi ya shilingi milioni 18 kwa mwezi kwa kila mmoja.
Chanzo cha taarifa hiyo kimesema: “Mara nyingine mapacha hawa hawalali kwa wakati mmoja, kwahiyo Beyonce aliamua kuajiri wafanyakazi watatu kwa kila mtoto mmoja, kila mmoja anafanya kazi saa nane kwa siku kwa kupokezana.”
Pia kuna wafanyakazi wawili kwa ajili ya dada yao (mtoto wa kwanza kwa Beyonce na Jay z), Blue Ivy, mwenye umri wa miaka mitano. Hii inafanya idadi ya wafanyakazi wa kuwahudumia watoto wa wanamuziki hao kuwa nane wanaofanya kazi mchana na usiku.
Imedaiwa kuwa wanandoa hawa wamekuwa wakiishi kwenye nyumba ya kupanga mjini Malibu mpaka walivyofanikiwa kupata jumba la kifahari jijini Los Angeles, ambalo lina nafasi kubwa ya kuweza kuishi na wafanyakazi hao wote.
Hii inamaanisha Beyonce na Jay Z wataongeza walinzi, magari yasiyopitisha risasi, na manesi wanaofanya kazi kwa saa 24 kwa kupokezana.
Mpaka sasa, Rumi na Sir wameshapatiwa mshauri wa masuala ya uwekezaji na fedha kwa ajili ya kuwaandalia mpango wao wa fedha kimaisha kwa majina yao wenyewe.
Pia wameshaajiri mtaalamu kuwaandalia majina watakayotumia kwenye mitandao ya kijamii na ‘hashtag’ kwa ajili yao.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post