BILA RONALDO, URENO YAICHAPA MEXICO, YASHIKA NAFASI YA TATU KOMBE LA MABARA

Timu ya taifa ya Ureno imefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Mabara kwa kuifunga Mexico mabao 2-1 katika mechi ya mshindi wa tatu iliyochezwa Jumapili hii.
Ureno imefanikiwa kuchukua nafasi hiyo ya tatu ikiwa bila nahodha wake, Cristiano Ronaldo ambaye alilazimika kuondoka kambini kutokana na kwenda kuangalia watoto mapacha aliowapata hivi karibuni.

Mexico ndiyo walioanza kufunga katika dakika ya 55 kutokana na Luis Neto kujifunga lakini beki wa Real Madrid, Pepe aliisawazishia Ureno katika dakika ya 90 na kufanya mchezo huo kuongezwa dakika 30.

Bao la ushindi lilifungwa na Adrien Silva dakika ya 104 kwa njia ya penalti baada ya mlinzi wa Mexico kuunawa mpira. Mchezo huo ulishuhudia kadi mbili nyekundu Nelsinho wa Ureno dakika ya 106 na Raul Jimenez wa Mexico dakika ya 112.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post