BOSI WA YANGA ATUA DAR, APOKELEWA NA MASHABIKI KIDUCHU

Kocha wa Yanga, George Lwandamina amerejea nchini Tanzania, leo Jumatatu akitokea kwao Zambia ambapo alikuwa huko kwa ajili ya mapumziko.
Lwandamina ametua mchana wa leo jijini Dar es Salaam ambapo alipokewa na Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere huku kukiwa na mashabiki wachache wa Yanga kwa kuwa ujio wake haukutangazwa.

Awali, ilielezwa kuwa kocha huyo anaweza kutorejea nchini kutokana na masuala ya kiuchumi kuwa tata ndani ya Klabu ya Yanga, tangu Yusuph Manji aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo kutangaza kujiuzulu.
Katika msimu wake wa kwanza akiinoa Yanga, Lwandamina ameiwezesha kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2016/18 licha ya kuwa aliingia wakati timu ikiwa katika mwendo baada ya kunolewa na Kocha Hans Van Pluijm ambaye kwa sasa ni kocha wa Singida United. 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post