DAKTARI AELEZA CHANZO CHA WANAUME WA DAR KUWA NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) amesema kuwa, asilimia 33 ya wanaume 672 wakazi wa Dar es Salaam wamebainika kuwa na upungufu wa nguvu za kiume.
Daktari Pedro Pallangyo aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema utafiti huo umefanyika JKCI ambapo kati ya wanaume watatu, mmoja aligundulika kukosa nguvu za kiume.
Pallangyo alieleza kwamba idadi kubwa ya wagonjwa wamebainika kuwa na shinikizo la damu na kisukari.
Utafiti huo ni miongoni mwa tafiti 16 zilizompa ushindi  wa tuzo ya Watafiti Vijana wa Afrika mwaka 2016/17 (Young Africa Research Awards 2017) zilizotolewa nchini Misri.
“Hali hii inaashiria kuwa magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu yamekuwa yakiongezeka mara kwa mara jambo ambalo linasababisha athari ya nguvu za kiume kuwa kubwa.”
Aidha, akielezea ufumbuzi wa tatizo, Pallangyo alisema, “Changamoto hivyo inaweza kutatuliwa iwapo jamii itakuwa na utaratibu ya kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kugundua tatizo mapema na kupata matibabu.”
Dk Pallangyo alisema kuwa, kati ya Machi mwaka jana hadi Machi mwaka huu alifanya tafiti hiyo katika ripoti ya muda mfupi na muda mrefu.
Dk. Pallangyo ambaye ni Mtanzania wa kwanza kupata tuzo hiyo anatarajia kukabidhiwa na Rais wa Misri, Abdi El-Fatah Al Sis mwezi  Agosti mwaka huu.
-MTANZANIA
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post