DALILI TANO KWAMBA UNAFANYA KAZI NA BOSI MZURI

SHARE:

Majukumu ya uongozi makazini yamekuwa yakibadilika hasa katika miaka michache iliyopita. Ni watu wachache wameweza kugundua hili mpaka sa...

Majukumu ya uongozi makazini yamekuwa yakibadilika hasa katika miaka michache iliyopita. Ni watu wachache wameweza kugundua hili mpaka sasa, lakini majukumu ya uongozi mwanzoni ilikuwa ni kulinda utawala na kusimamia sheria na taratibu. Mameneja walikuwa na jukumu la kuhakikisha wafanyakazi wanatimiza malengo ya kampuni na mara nyingi bila kujali kuhusu kuwawezesha, kuwahusisha au kufanya lolote kuhusu maendeleo ya wafanyakazi wake. Sasa mambo yamebadilika na yanaendelea kubadilika kwa kasi. Majukumu ya uongozi sasa yamebadilika, na zifuatazo ni dalili tano kwamba unafanya kazi chini ya bosi mzuri:
Anakuwa kama kocha
Makocha na walimu ni huhamasisha maendeleo ya watu wengine. Hutusaidia wakati wote maishani mwetu, iwe kwenye michezo au matibabu. Hii ndio sababu ya kuhitaji kuwa na kocha mahala pa kazi na mtu bora zaidi kuichukua nafasi hii ni meneja wako. Mameneja wazuri zaidi huhamasisha wafanyakazi wake kutimiza malengo yao kama ambavyo mwalimu wa michezo anafanya. Mameneja wa aina hii wana upeo wa kuona thamani yako mbali na kazi aliyokupa na kutaka mafanikio ya wafanyakazi wake. Viongozi wa namna hii wanaamini katika kuwainua wafanyakazi wake, kuwasaidia kutatua matatizo yao na kuwawezesha wapate mafanikio zaidi.
Anayaelewa mapungufu yako lakini anajali zaidi unayoyamudu
Ni rahisi sana kuona mapungufu ya mtu. Kama jambo halikwenda kama lilivyopangwa, ni rahisi kulaumu wengine. Ni ngumu kuangalia nje ya mapungufu ya watu na kuzingatia ubora na vipaji vyao halisi. Hii haimaanishi udharau mapungufu waliyonayo wafanyakazi – kinachomaanishwa ni kwamba kuelewa kwamba mapungufu yapo lakini anaamua kuwekea mkazo kwenye mambo unayoyaweza. Mameneja wazuri wanaelewa uwezo wa wafanyakazi wao na wanawahamasisha watumie vipaji vyao. Hili linaonekana sana kwenye michezo yote ambapo kocha humuweka mchezaji kwenye nafasi ambayo itampa mafanikio zaidi. Hili linahitajika zaidi makazini na mameneja ndio walitekeleze.
Anataka kujua historia yako
Kila mtu ana historia ya maisha toka utotoni mwake mpaka alipofikia sasa, mambo anayothamini na jinsi anavyotaka maisha yake yawe. Hadithi ya maisha yako ndiyo inakuelezea zaidi na mameneja bora wanapenda kuisikia toka kwako kwakuwa wanahitaji kumjua mtu zaidi ya kuwa unafanya kazi kwenye kampuni yake. Wanaweza kufanya hivi kwa kukuuliza tu “unaendeleaje?” au kuwachukua wafanyakazi wake na kwenda sehemu kuzungumzia mambo tofauti yasiyohusu kazi. Kwa mameneja, kujenga uhusiano wa namna hii na wafanyakazi wake ni muhimu sana, kwahiyo kama meneja wako yupo hivi, jihesabu mwenye bahati.
Wanatambua mapungufu yao
Mameneja wazuri wanakubali mapungufu yao na hawapendi kuigiza kujua kila kitu maishani. Wanahitaji kujua hadithi za wafanyakazi wao na pia hawaogopi kuhadithia historia za maisha yao ili wafanyakazi waweze kumjua vizuri zaidi. Mara nyingi tumesikia habari mameneja wakishuhudiwa kufanya jambo moja wakiwa mtaani na kubadilika kuwa mtu tofauti kabisa akiwa ofisini, anageuka kuwa roboti asiyetaka ushauri wa mtu – na watu hawapendi kufanya kazi na roboti, wanataka kufanya kazi na mtu anayetambua kwamba yeye si mtimilifu.
Huukosoa utaratibu uliozoeleka wa kufanya kazi
Maya nyingi makazini mwetu, taratibu na mbinu za kufanya kazi zimekuwa ni zile zile kwa miongo migi sana wakati dunia imebadilika sana katika miaka michache iliyopita lakini taratibu za utendaji kazi hazibadiliki kuendana na mabadiliko ya wakati. Ni sawa na kuishi mwaka 2017 lakini tunafanya kazi kwa taratibu zilizokuwa ni sahihi miaka ya 1970. Mameneja wazuri wanaelewa kuwa mara nyingine kuleta mabadiliko ni jambo zuri kuliko kuyazuia yanapotokea. Mameneja wa aina hii hawaulizi tu swali, “kwa nini tunafanya namna hii?” bali wanahamasisha wafanyakazi wawe wabunifu na kuja na mbinu mpya zitakazoboresha utendaji. Mabadiliko haya yaweza kuwa ni kuanzisha utaratibu mpya, matumizi ya teknolojia mpya au kubadilisha mpamgilio wa vitu ndani ya ofisi, mameneja wazuri huwa ni lazima watabadili taratibu zilizozoeleka!

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: DALILI TANO KWAMBA UNAFANYA KAZI NA BOSI MZURI
DALILI TANO KWAMBA UNAFANYA KAZI NA BOSI MZURI
https://3.bp.blogspot.com/-5zlIudAlCac/WWuVaBGxVdI/AAAAAAAAc1s/rTcwFYFPWCUGJBmF83SycfQnL1KbqmfYACLcBGAs/s1600/xvf-698x375.jpg.pagespeed.ic.L20RG1898v.webp
https://3.bp.blogspot.com/-5zlIudAlCac/WWuVaBGxVdI/AAAAAAAAc1s/rTcwFYFPWCUGJBmF83SycfQnL1KbqmfYACLcBGAs/s72-c/xvf-698x375.jpg.pagespeed.ic.L20RG1898v.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/07/dalili-tano-kwamba-unafanya-kazi-na.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/07/dalili-tano-kwamba-unafanya-kazi-na.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy