DAWASCO YATANGAZA KUKATA MAJI SIKU NZIMA JULAI 31

UBORESHAJI WA MTAMBO MPYA WA UZALISHAJI MAJI WA RUVU JUU.
Shirika Ia Maji Safi na Maji taka Dar-es-salaam (DAWASCO), Iinawatangazia wateja wake wote wa jiji la Dar es-salaam pamoja na Mji wa Kibaha Mkoani Pwani kuwa mtambo wa uzalishaji Maji wa Ruvu Juu utazimwa kwa wastani wa Saa 8, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni, siku ya Jumatatu tarehe 31/07/2017.
Sababu ya kuzimwa kwa Mtambo: Kumruhusu Mkandarasi (WABAG), kukamilisha Mfumo wa umeme katika mtambo mpya wa uzalishaji Maji wa Ruvu Juu uliopo Mlandizi mkoani Pwani.
Maeneo yatakayoathirika na Kuzimwa Kwa Mtambo huu:
Mlandizi Mjini, Ruvu Darajani, Vikuruti, Disunyara, Kilangalanga, Janga, Mbagala, Visiga, Maili 35, Zogowale, Misugusugu, Tanita, Kibondeni, Kwa Mathias, Nyumbu, Msangani, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Sofu. Lulanzi, Gogoni, Kibamba, Kibamba Njia Panda Shuel Kibwegere, Mloganzira, Kwembe, Kibamba Hospitali, Kwa Mkinga, Luguruni, Kimara, Ubungo,na baadhi ya maeneo ya Tabata.
Toa taarifa Dawasco kupitia vituo vya wateja Dawasco kimara 0743-451865,Dawasco Tabata 0743-451867, Dawasco Kibaha 0743-451875
Dawasco inawaomba wateja kutunza Maji ya kutosha pindi Mtambo utakapokamilika.
Kwa taarifa zaidi wasiilana nasi: Kituo cha huduma Kwa wateja 0800110064 (BURE) au Tembelea: www.dawasco.go.tz
lmetolewa Na:
Ofisi Ya Uhusiano Dawasco-Makao Makuu
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post