DIAMOND AWACHANA WANAOMSEMA ZARI KUHUSU MSIBA WA MAMA YAKE

Mwanamuziki Nasib Abdul, maarufu kwa jina la sanaa la Diamond Platnumz amewachana wabongo wanaomsema mzazi mwenzake Zari The Boss Lady kuhusu alivyojiweka katika kipindi chote cha msiba wa mama yake mzazi.
Zarinah Hassan ambaye alifiwa na mama yake Julai 20 mwaka huu amekuwa akisemwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa hakuonyesha kuhuzunika na tukio hilo na kwamba aliishia kujiremba mithili ya bibi harusi.
Aidha, wengine walisema kuwa hata siku ya mazishi ya mama yake, Zari hakutoa chozi kuonyesha kuwa amesikitisha na kuondokewa na nguzo hiyo muhimu katika maisha yake.
Kuonyesha kukerwa na hayo yote, mwanamuziki Diamond amewataka watu hao wamuache mpenzi wake huyo, kwani hawezi kukaa ndani na kulia ili awaonyeshe watu kuwa amepatwa na matatizo.
“Kuna vi***pi kunuka wanajifanya wanajua sana uchungu wa Misiba ya watu…. Mtoto wa watu katoka katika matatizo mfululizo, anatakiwa apelekwe sehem tulivu apetiwepetiwe adekezwe apate faraja!…sasa kama nyie hamna mabwana wa kuwafanyia hayo, Msijifanye ni Tamaduni na kulazimisha kila mtu awe kama nyie, eti kutwa nzima ajifungie chumbani kulia…”
Diamond alisema kwamba ana siku tano za kukaa na mzazi mwenzake huyo ili kuweza kumfariji kutokana na kupitia kipindi kigumu, ambapo mbali na kufikwa na mama yake, Mei 25 mwaka huu, mzazi mwenzake, Ivan Semwanga alifariki dunia.
“Nina siku 5 za kumpetipeti… leo ndio kwanza Ya kwanza ๐Ÿ˜›

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post