DUDU BAYA AMFANANISHA NEY WA MITEGO NA GIGY MONEY, AMBER LULU

Msanii Mkongwe wa muziki wa hip hop, Dudu Baya amemfananisha rapa Nay wa Mitego na Gigy Money na Amber Lulu kwasababu muziki wao umetawaliwa na majungu na majigambo.
Dudbaya amesema yeye binafsi sio mshabiki wa muziki wa Nay wa Mitego kwasababu muziki wake haueleweki na ndio maana anamfananisha na Amber Lulu na Gigy Money.
“Kuna wasanii wakali wanafanya muziki mzuri kuliko huyo lakini hawapewi support, mimi ningewashauri tu mashabiki wa muziki wapende muziki mzuri,” amesema Dudu.
Amesema hajui rapa huyo anafanya muziki wa namna gani kwani amekuwa ni msanii wa hip hop anayetumia mwamvuli wa hip hip kuwasema watu.
Mkongwe huyo amewataka mashabiki wa muziki kusikiliza muziki mzuri ambao utawajenga na sio muziki ambao ndani yake una maneno ya kuwasema watu bila sababu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post