FAIZA: KUMUONESHA BABA KIJACHO KWANGU NOO!

Mrembo kunako Bongo Muvi ambaye pia ni mzazi mwenzie na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally amefunguka kuwa kati ya vitu ambavyo havipendi katika ujauzito wake huu ni kumuanika baba kijacho wake.

Akionyesha kibendi chake.

Akipiga stori na Star Mix, Faiza alisema kuwa, anafurahi kuwa mama mtarajiwa wa mtoto wake pili lakini linapokuja suala la kupiga naye picha ama kumuanika baba kijacho wake mitandaoni kama wafanyavyo wasanii wengine kwake halina nafasi.
Akijiachia ufukweni.

“Kwanza nalipenda tumbo langu likiwa imejaa (ujauzito) lakini pia hakuna kitu ninachokiogopa kwa sasa kama kumuanika baba kijacho wangu ambaye yupo nje ya nchi kwa sasa naogopa wasije mkwapua bure, hayo mambo sijui ya kuuza sura naawaachia hao wasanii wengine,” alisema Faiza ambaye mtoto wake wa kwanza amezaa na Sugu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post