HATIMAYE CHICHARITO ATAMBULISHWA KUWA MCHEZAJI WA WEST HAM

Klabu ya West Ham United imekamilisha mchakato wa kumsajili mshambuliaji Javier Hernandez maarufu kwa jina la Chicharito kwa ada ya pauni milioni 16 akitokea Bayer Leverkusen ya Ujerumani.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United, amekamilisha usajili huo na atakuwa akilipwa pauni 140,000 kila wiki katika mkataba wa miaka mitatu.
Akiwa Man United, Chicharito alisifika kwa kufunga mabao katika mazingira mazuri na hata hivi karibuni kocha wa sasa wa United, Jose Mourinho aliwahi kumzugumzia kwa kumsifia kuwa ni mmaliziaji mzuri awapo mbele ya lango.
Chicharito alifanyiwa vipimo vya afya jana na kukamilisha dili hilo leo Jumanne ambapo baada ya hapo atasafiri kuelekea Ujerumani kuungana na wenzake ambao wapo nchini humo kwa ajili ya mechi za kirafiki.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post