IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO JESHI LA POLISI, KAMANDA MPINGA AHAMISHIWA MBEYA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Saimon Sirro, amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani pamoja
na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya.
Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Naibu Kamishna wa Polisi Mohamed Mpinga anaenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu.
Aidha, Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya (DCP) Dhahiri Kidavashari amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi.
Uhamisho huo ni wa kawaida katika kuboresha utendaji wa kazi za Polisi kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.
Imetolewa na:
Barnabas D. Mwakalukwa – ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post