JESHI LA TAIFA STARS LIKO FITI KUWAVURUGA WAZAMBIA

Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga amesema kikosi chake kipo kamili kuikabili Zambia kufuzu fainali michuano ya COSAFA Afrika Kusini mchezo ambao unatarajiwa kuchezwa leo Jumatano jioni.
Taifa Stars inatarajiwa kushuka uwanjani kuivaa Zambia katika nusu fainali ya COSAFA, inayoendelea nchini Afrika Kusini, ikiwa imefika hatua hiyo baada ya kuwatoa wenyeji ambao pia walikuwa mabingwa watetezi, Afrika Kusini kwa ba 1-0, bao likifungwa na mshambuliaji Elias Maguri dakika ya 17.

Mayanga amesema mchezo utakuwa mgumu lakini amekiandaa vyema kikosi chake kuhakikisha wanaibuka na pointi tatu kwenye mchezo huo ambao wameupa umuhimu mkubwa.

Amesema ukimtoa mshambuliaji Mbaraka Yusuph, wachezaji wengine wote wapo fiti kwa ajili ya mchezo huo na anahakika watapambana kwa nguvu zao zote ili kupata ushindi.

Kocha huyo amesema timu yake imekuwa ikibadilika katika kila mchezo na hiyo inatokana na wapinzania wao wanavyocheza ndiyo na wao wanabadilika kuendana na presha ya mchezo ilivyo hivyo amewataka Watanzania kuondoa hofu na kuwaombeea dua ili waweze kushida.

Zambia ilitinga hatua hiyo kwa kuitoa Botswana kwenye robo fainali, hivyo mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kwani timu zote zimekuwa na ushindani mkubwa ingawa Zambia wapo juu kwenye viwango vya FIFA, ukilinganisha na Tanzania.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post