JINSI O.J SIMPSON ALIVYOTENGENEZA ZAIDI YA BILIONI 1.3 AKIWA GEREZANI

Inasemekana kwamba O.J. Simpson, ambaye anatakiwa kuruhusiwa kurudi uraiani kwa mpango wa ‘parole’ kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu, amekuwa akijiingizia kipato cha dola za Marekani 10,565 (sawa na shilingi milioni 23.7) kila mwezi kwa miaka mitano aliyokaa gerezani, alipoingia akiwa na miaka 65.
Hiyo ni kwa sababu O.J ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 70 atakuwa akipata pesa za mafao yake yanayotokana na uwekezaji wake aliokuwa akiufanya kwenye chama cha ligi ya mpira wa miguu nchini Marekani (NFL) ambayo baada ya mzozo mrefu na wanasheria wameamua kumruhusu achukue zaidi ya dola za Marekani 600,000 (zaidi ya shilingi bilioni 1.3) pesa ambayo hakuruhusiwa kuitoa kutokana na kuwa gerezani kwa miaka mitano iliyopita. Jarida la ‘USA Today’ liliripoti kuwa Mwanasheria wa Simpson amesema kuwa staa huyo wa zamani wa filamu ana pesa zinazotokana na mafao yake yanayotokana na uwekezaji wa dola za Marekani milioni 5 alioufanya miaka mingi iliyopita.
Kwa mujibu wa NFL, mahesabu ya pensheni yanatokana na misimu ya ligi iliyochezwa na umri ambao muwekezaji anaamua kuanza kuchukua pesa yake. Simpson aliwekeza katika misimu ya ligi kuanzia mwaka 1969 mpaka mwaka 1979, na alisema atasubiri mpaka atakapofikia miaka 65, sio miaka 55, ndio ataanza kuchukua pensheni yake.
Kiasi hiki cha pesa ambacho O.J kwa sasa anaruhusiwa kupokea kila mwisho wa mwezi kutokana na uwekezaji kwenye mpango wake wa mafao ya uzeeni, ni kikubwa kwa kipimo chochote kile kwakuwa wachezaji wengi wa ligi hiyo huwa hawapati kiasi kikubwa kama hicho cha mafao kila mwezi. Mchezaji wa kawaida wa ligi hiyo hudumu misimu mitatu tu na kutokana na matumizi mabaya, wengi wao hujikuta wakianza kutumia pensheni yao mapema zaidi kutokana na ukata. Wachezaji wengi wastaafu wa ligi hiyo ya NFL walishatangaza kufilisika.
Ligi hiyo kwa sasa inaruhusu wachezaji kujiwekea kwenye mfuko wa pensheni kwa muda wote watakaokuwa wanacheza ili kuwahamasisha wachezaji waweze kutunza pesa wanazolipwa. Kwa pesa ambayo mchezaji ataweka kwenye pensheni yake, ligi hiyo huongezea zaidi ya dola 36,000 (zaidi ya shilingi milioni 80), ikimaanisha kwamba mchezaji anakuwa anastahili kupata mara tatu ya kiasi alichojiwekea kama akiba yake kwenye mfuko wa pensheni.
Pensheni ya Simpson inaonekana kuwa kubwa sana kuwazidi wachezaji wastaafu wa ligi hiyo lakini ana madeni makubwa sana. Baada ya kumuua mkewe mwaka 1995, Mahakama iliamua katika kesi dhidi yake kwamba ailipe familia ya mkewe huyo kama adhabu na fidia kiasi ambacho pamoja na malimbikizo sasa kinafikia dola za Marekani milioni 52 (zaidi ya bilioni 116), lakini imekuwa ni bahati nzuri sana kwa Simpson kwani kwa mujibu wa Sheria za nchi hiyo, si lazima atumie pesa hizi kulipia deni lake.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post