JOHARI: SIJAWA ‘USED’ BADO NINAHESHIMIKA

Blandinda Chagula ‘Johari’ .

STAA wa filamu za Kibongo toka kitambo, Blandinda Chagula ‘Johari’ ametema cheche kuwa hata kama ametumika muda mrefu kwenye tasnia hiyo lakini bado anaheshimika kwa mashabiki wake na siyo ‘Used’ kama wanavyodai mastaa wanaochipukia.

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Johari ambaye jana Ijumaa Julai 28, 2017 ilikuwa ni kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa, alisema anaamini yeye kama staa aliyekuwa akisumbua huko nyuma anapotumia akili au kuweka jambo lolote kwenye filamu hata kama hataicheza yeye bado itakuwa na ladha nzuri ya kipekee.

“ Yaani utasikia hawa mastaa wapya wanapenda kutuita sisi ni ‘Used’ lakini ukweli ni kwamba japokuwa wanatuita hivyo ladha ya mastaa wa zamani ni tofauti na wa sasa, kuna vitu ukiviangalia hatuwezi kulingana kabisa,” alisema Johari.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post