JOHN TERRY AIKIMBIA PREMIER LEAGUE, ASAINI ASTON VILLA

Nahodha wa zamani wa Chelsea na England, John Terry amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Klabu ya Aston Villa inayoshiriki Championship.
Mmiliki na Mwenyekiti wa Villa, Dr Tony Xia alithibitisha kuwasili kwa staa huyo aliyepata mafanikio makubwa akiwa na Chelsea, Jumatatu asubuhi

Awali iliaminika kuwa Terry atajiunga katika timu yoyote ya Premier League lakini imekuwa kinyume chake.

Kuwasili kwa Terry ambaye alikuwa anawindwa pia na mahasimu wa Villa, Birmingham City kuliwafanya mashabiki wa klabu hiyo kuanzisha group maalumu la WhatsApp kwa ajili ya kumkarubisha mchezaji huyo ambaye ana umri wa miaka 36.

Terry ameichezea Chelsea kwa miaka 22 lakini aliondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu uliopita.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post