KAFULILA ALIVYOPOKEA SIFA ZA RAIS DKT MAGUFULI

Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, David Kafulila (sasa yupo CHADEMA) amesema kuwa amefurahishwa na kauli ya Rais Dkt Magufuli aliyoitoa mwishoni mwa wiki ambapo alionyesha kuunga mkono jitihada zake za kupambana na ufisadi nchini.
Kafulila ameyasema hayo ikiwa ni siku moja tangu Rais Magufuli alipommwagia sifa kwa jinsi alivyosimama kidete na kupambana katika sakata la Escrow lililosababisha serikali kupoteza mabilioni ya fedha.
Rais Magufuli aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Nguruka katika hafla ya uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji uliopo Tarafa ya Nguruka katika Wilayani Uvinza ambapo alisema kuwa akiondoka hapo bila kumpongeza Kafulila atakuwa amefanya dhambi ya unafiki itakayompeleka motoni.
Rais Magufuli alisema kuwa licha ya kuwa Kafulila alikumbana na vitisho mbalimbali wengine wakitaka hata kumshtaki pamoja na kutukanwa kwa kuitwa tumbili lakini aliendelea kupambana akiwatumikia waatanzania kwa ujumla.
Kafulila alisema kwamba, amefarijika sana kuona Rais wa nchi ametambua juhudi zake alizozifanya katika kupambana katika sakata la ufisadi la IPTL/Escrow na kwamba hatua hiyo inamtia moyo kuendelea kulinda maslahi ya watanzania.
Kafulila ambaye alishindwa kutetea kiti chake cha ubunge na jimbo hilo kwenda mikononi mwa CCM, alisema katika kipindi chote cha mapambano katika vita hiyo alikumbana na changamoto mbalimbali zilizolenga kumkatisha tamaa, lakini aliendelea kupambana akijua kuwa anafanya kwa niaba ya watanzania.
Kuhusu jitihada za Rais Magufuli katika kupambana na ufusadi, Kafulila alisema kwamba anamuunga mkono na kwamba anaamini watu wote waliohusika kwenye wizi wa fedha za umma mbali na sakata la Escrow nao wanashughulikiwa.
Lakini pia Kafulila alimuomba Rais Magufuli kuhakikisha kuwa anaweka taasisi na mifumo imara itakayoendelea kupambana dhidi ya ufisadi hata baada ya yeye kuondoka.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post