KATIBU MKUU WA CHADEMA NA WABUNGE WAWILI WAKAMATWA

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji, Mbunge wa Jimbo la Ndanda, Cecil Mwambe ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kusini pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma, Zubeda Sakuru wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Mbamba Bay mkoani Ruvuma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama hicho, viongozi hao wamepelekwa kituoni kuhojiwa ambapo Katibu Mkuu Dkt. Mashinji ametakiwa kueleza kwanini yuko Mbamba Bay na aeleze amekwenda kufanya nini.
Polisi wamemkamata Katibu Mkuu Dkt. Mashinji, Mbunge Mwambe na Mbunge Zubeda baada ya kuvamia kikao cha ndani kilichokuwa kikiendelea mjini hapo ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu Dkt. Mashinji kukagua shughuli za chama katika majimbo ya kanda hiyo iliyoanza leo, ilieleza taarifa.
Msemaji wa CHADEMA, Tumain Makene amesema kuwa chama hicho kitaendelea kutoa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post