KERO ZINAZOLETWA NA WATALII WANAPOTEMBELEA MATAIFA MENGINE

Watalii huwa wanajipatia sifa mbaya ingawa kuwa mtalii inaweza kuwa ni jambo zuri sana – lakini inabidi kuheshimu tamaduni ya watu wa sehemu unayokwenda kutalii. Lakini kwa bahati mbaya sana si kila mtalii anafanya hivyo.
Ukurasa wa Quora uliuliza, “NI vitu gani vinavyokera zaidi vinavyofanywa na watalii kutoka nje ya nchi wanaokuja nchini kwenu?” swali hili likasababisha watu wengi kutapika nyongo zao.
Haya ni mambo ambayo watalii wamekuwa wakiyafanya kwa kujirudia rudia kwenye nchi 14 ambavyo vimekuwa ni kero kubwa kwa wenyeji wa nchi husika:

Denmark: Watalii kutotumia barabara sahihi

Watalii wamekuwa wakidharau au kutoheshimu alama zilizowekwa barabarani nchini Denmark zinazotofautisha sehemu ya waenda kwa miguu na wapanda baiskeli wakiwa kwenye barabara kuu. “Majira ya kiangazi kila mwaka, mitaa ya Mji Mkuu wa nchi hiyo, Copenhagen inajaa watalii ambao wanalaumiwa kwa kutochukua hata dakika tano tu za kuyasoma mazingira waliyopo ili waone mpangilio huu uliowekwa na kusababisha watembee kwenye sehemu ya wapanda baiskeli wakiwa na mabegi yao makubwa, wakiwa wanasimama mara kwa mara kupiga picha – jambo linalowakera wenyeji wa jiji hilo.
Jambo jingine ni watalii wanaokodisha baiskeli ambazo taa zake zinazotakiwa kutoa ishara hazifanyi kazi. Wenyeji wanasema hili ndio jambo baya zaidi.
Mmoja wa wananchi wa jiji hilo amesema: “Kama umekodisha baiskeli ili kutalii mitaa ya jijini Copenhagen (jambo ambalo unashauriwa sana ulifanya ili kujua sehemu nyingi) na huzingatii kama taa za ishara zinafanya kazi, au unaendesha baiskeli hiyo bila kutoa ishara, nakuchukia sana.”

India: Watalii kupiga picha maskini kwa kuwapiga picha

Wenyeji hawapendi tabia ya watalii “kudhihaki maskini” kwa kwenda kwenye maeneo ya watu maskini bila ruhusa wakiwa na kamera zao za bei ghali – jambo linalochukuliwa kama kupima imani za watu. Wenyewe wanasema kuwa sehemu hizo si mbuga za wanyama kwamba mtalii ajiamulie tu kupiga picha watoto anaowaona bila kuruhusiwa au kuzurura mitaani wakitafuta maskini wengine wa kuwapiga picha wakati wenyeji wanakuwa wanadhihakiwa majumbani mwao ambapo ndipo wanapoendesha maisha yao ya kila siku.
Pia, wengine wanachukia sana pindi watalii wanapokuja nchini India kujifunza “Yoga bila kufuata misingi kwa lengo la kujua njia za kufanya mapenzi kwa tamaduni za nchi hiyo na kufata watu wanaojiita wataalamu au wakongwe ambao hawajui kitu juu ya wanachokifundisha.
Wataalamu hawa ambao wanakuwa wamewasiliana na watalii hao kabla hawajafika nchini India mara nyingi ni feki na hawajui kabisa taaluma wanayoifundisha. “Wataalamu” hawa hawajui chochote kuhusu jinsi ya kufanya ‘meditation’ kama inavyotakiwa kwenye yoga, na kwamba matapeli hao wameifanya yoga kuwa biashara kwao na si mfumo wa maisha unaomuongezea mtu amani kama ulivyokusudiwa.
Inawakera wenyeji wanaapoona watalii wanaofika nchini humo kwa lengo la kuelimishwa mbinu za kuwa na amani zaidi na kujikuta wakiishia mikononi mwa matapeli hawa na ‘wataalamu’ wa biashara ambao wanachofanya ni kuwafundisha jinsi ya kuvaa nguo za kiasili za Kihindi, kufanya mapenzi kwenye maeneo ya wazi na kunywa dawa ili kujisikia una amani zaidi.

Italia: Watalii kutofata Sheria za nchi

Wageni wanaamini kabisa kwamba nchi ya Italia ni nzuri sana na haina sheria kabisa, na wanadhani kwamba wanaweza kujiamulia kufanya kila wanachojisikia kufanya. Inabidi kila anayekwenda kufanya utalii nchini humo ajue kwamba jambo hili si kweli. Mfano ni kwamba haruhusiwi kuoga. Huruhusiwi kuoga kwenye bwawa la Trevi. Huruhusiwi kukojoa kwenye vichochoro vya mitaa kwa sababu tu ni usiku na huonekani. Haruhusiwi kuparamia masanamu ambayo yanahusishwa na kumbukumbu kubwa ya historia ya nchi hiyo (walioyatengeneza ni wasanii wakubwa wa nchi hiyo wakiwemo Bernini, Canova na Michelangelo, kwahiyo wenyeji wanahitaji watu hao wapewe heshima inayostahili kwenye kazi walizozifanya).
Pia huwa ni kero kubwa sana kwa wenyeji pale watalii wanapokuwa nchini Italia na kudhani kila mmoja anaweza kuongea Kiingereza na kujikuta wakiwa migahawani wanaagiza vyakula vya asili ya Italia lakini wanataka vipikwe kwa mapishi ya tamaduni walizotoka.

Indonesia: Watalii kuombaomba

Watalii kutoka nchi za Magharibi huwa mara nyingi wanaonekana wakiwa wanaombaomba ili kupata pesa za kutalii. Kama jambo hili si kero basi sijui liitwe vipi kwakuwa ni kitu kibaya kwa wao kutalii ‘uswahilini’ na sehemu zenye nyumba zilizofungamana kwenye nchi mbalimbali na kuanza kuwapiga picha ombaomba, lakini wanapoamua kuungana nao na wao kuanza kuomba ili wapate pesa ya kumalizia likizo zao inakuwa ni kuvuka mipaka ya wanachotakiwa kukifanya.
Ujerumani: Kupiga picha za ‘selfi’ kwenye maeneo ya kumbukumbu za wahanga wa utawala wa Nazi
Sarah Freytag ambaye ni mkazi wa jijini Berlin huwa anashindwa kuvumilia akiona watalii wanapiga picha za ‘selfi’ kwenye makumbusho ya kumbukumbu ya waliouawa kipindi cha utawala wa Nazi au “kumbukumbu za wahanga wa utawala wa Nazi.” Anasema kwamba, kibaya zaidi ni pale wengine “wanapokaa ‘mikao ya ajabu’, kuonesha ishara za ushindi kwa vidole, au ishara za kitu kizuri (au kibaya, haijalishi) kwa kuiga ishara za Hitler.”

Thailand: Kupiga picha na chui waliopewa dawa za kuwalevya

Wakazi wa jijini Bangkok, Thailand wanachukizwa sana pale watalii wanapokuwa wanapiga picha na chui waliopewa dawa za kuwalevya. Kitendo cha kutumia wanyamapori kama vipendezesha picha ili kujiongezea umaarufu kwenye akaunti zako za mitandao ya kijamii ni jambo linalokera sana wenyeji bila kujali kwamba wanaweza kuwa wanakuangali huku wakitabasamu.
Wengi wao wanasema kuwa kuwatumia wanyamapori kama vivutio vya utalii ni zaidi ya maagizo ya watalii hao kwamba watakudhuru, na dawa wanazowapa ni ukatili dhidi ya wanyama.

Norway: Kwenda karibu sana na milima ya barafu zaidi ya inavyotakiwa

Milima ya barafu nchini Norway imewekewa uzio na mabango yanayoonesha onyo kwa sababu maalumu — kwa sababu mara nyingi watu huwa wanafariki kwenye milima hiyo.
Watu wengi wanajua kwamba mito ya asili huwa ni hatari na inaua, inabidi waelewe kwamba maeneo ya asili yaliyowekewa uzio nchini Norway, inamaanisha kuwa maeneo hayo yana hatari kubwa sana zaidi ya inavyoweza kufikiriwa. Kwahiyo, kwa ajili ya wote unaowapenda maishani mwako, kaa katika upande sahihi wa uzio kwenye milima hiyo.

Uingereza: Watalii kuongea kwa sauti ya juu kwenye treni

Wageni huwa wanawakera sana wenyeji wa Uingereza kwa tabia ya kuongea kwa sauti ya juu wakiwa kwenye treni, hasa katika muda wa msongamano mkubwa wa watu wanaosafiri. “Waingereza si kwamba wanapanda treni ili kufurahia mazingira kama ilivyo kwa watalii. Wengi wao wanadai kuwa watu zaidi ya asilimia 50% wanakuwa na uchovu kutokana na pombe wanazokunywa. Waingereza mara nyingi hawapendi kuongea (au watu wanaoongea kwa sauti ya juu), hivyo kuwataka watalii wanaotembelea nchi hiyo kuwa kimya wanapokuwa ndani ya treni.

Australia: Kuendesha gari upande usio sahihi wa barabara

Wananchi wa Australia huwa wanakwazika pale wageni wanapoendesha gari kwenye upande wa barabara ambao si sahihi. Nchini Australia, dereva unatakiwa utumie upande wa kushoto wa barabara. Nchi zinazotumia upande wa kulia ni nyingi zaidi kuliko zile zinazotumia upande wa kushoto, kwahiyo ni hatari kwa dereva aliyezoea kuendesha gari kwenye nchi hizo anapotaka kuendesha gari nchini Australia.
Mara nyingine watalii huwakera zaidi wenyeji wanaposema “watu wa Australia wanaendesha gari kwa kutumia upande tofauti wa barabara,” wakati jibu ni hapana – wao (watalii ndio wanaoendesha gari upande ambao si sahihi.

Marekani: Kuwashangaa watu wa kabila la Amish

Wenyeji wanasema kuwa ni kero kubwa mtalii akiwa anawashangaa watu wa kabila la Amish kwakuwa huwa hawapendi kupigwa picha. Kwahiyo kama ukifanya utalii kwenye maeneo ambayo watu wa kabila hili wapo, jizuie kupiga picha au upige utakapokuwa umeruhusiwa tu. usiwaangalie wala kuwashangaza, hawapendi!

Croatia: Kupiga ‘selfi’ kwenye safu ya mito Plitvice


Wenyeji wanalalamika kwamba ingawa watalii wamekuwa wakionywa mara kwa mara waache kupiga ‘selfi’ katika safu za Hifadhi ya Taifa ya mito Plitvice, bado wamekuwa wakiendelea kufanya hivyo bila kujali. “kufanya hivi ni hatari kubwa kwao kuliko kero wanayoisababisha. Watalii wengi wameshakutwa wamekufa au wakiwa wamejeruhiwa wakati wanajipiga picha wakiwa kwenye vilele au karibu na vilele vya vilima. Hakuna picha yenye thamani kubwa zaidi ya maisha yako.

New Zealand: Kudhani kwamba hakuna mtu anayeelewa unachosema

Wageni wengi sana wanadhani kwamba wenyeji hawajui lugha ya Kiingereza na wanakuwa wanaongea upuuzi na kashfa kwa sauti ya juu kabisa. Watu wa Taifa hili wanaoweza kujua lugha zaidi ya moja wanaongezeka kwa wingi. Tahadhari ni kwamba unaweza kuwa unatoka sehemu yoyote duniani ambayo unaweza kudhani kwamba hamna mtu anayemjua lugha unayoongea, lakini mtu aliyekuwa pembeni yako kwenye basi akawa anaelewa kabisa kashfa unazotoa.
“Tafadhali usiivalishe tabia yako nguo chafu kwenye kadamnasi ya watu. Utaumbuka!
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post