KESI YA MBOWE YA MADAI ZAIDI YA MILIONI 500 YAANZA KUSIKILIZWA

Mahakama Kuu kanda ya Moshi jana ilianza kusikiliza kesi inayomkabili Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa iliyofunguliwa na kampuni ya Kilimanjaro Veggies Ltd, inayomilikiwa na Freeman Aikael Mbowe.
Kampuni hiyo imemshtaki Mkuu huyo wa Wilaya kwa kushiriki kuharibu miundombinu ya shamba la mbogamboga lililokuwa katika kijiji cha Nshara kilichopo Wilaya Hai, shamba linalomilikiwa na Mbunge huyo na kumtaka Mkuu huyo wa Wilaya alipe fidia ya zaidi ya shilingi milioni 549 baada ya shamba lake kuvamiwa na miundombinu kuharibiwa.
Wakili wa Mbowe aliiomba Mahakama ifute zuio lililowekwa na Mkuu wa Wilaya kwamba shughuli za kilimo zisiendelee kwenye shamba hilo kwakuwa familia ya Mbunge huyo wamekuwa wakiendesha shughuli za kilimo kwenye eneo hilo kwa zaidi ya miaka 80 bila kuharibu mazingira. Shamba husika lililoharibiwa lina ukubwa wa ekari 2.7
Wakili wa Mkuu wa Wilaya huyo, Modestus Njau aliiomba Mahakama hiyo ikubali ombi la kumjumuisha katika kesi hiyo Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju kwakuwa mshtakiwa ni Mkuu wa Wilaya na huwa anashtakiwa kutokana na majukumu ya Serikali aliyokuwa akiyatekeleza.
Kwa mujibu wa Wakili huyo, Sheria ya TAMISEMI ya mwaka 1997, ibara ya 14, ibara ndogo ya kwanza na pili, vinataja kazi za Mkuu wa Wilaya na majukumu yake na kwamba majukumu hayo ndiyo yaliyosababisha afikishwe mahakamani.
Wakili anayeitetea kampuni ya Mbowe alikubaliana na ombi hilo kwa sharti la ombi hilo kuwasilishwa kwa maandishi. Jaji Sumari alimtaka wakili wa mshtakiwa awasilishe maombi hayo kwa maandishi na kuahirisha kesi hiyo mpaka Agosti 14 mwaka huu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post