KIONGOZI WA GENGE LA DAWA ZA KULEVYA ALIYEBADILI SURA KWA MIAKA 30 AKAMATWA

Kiongozi wa kundi la kihalifu la kusambaza dawa za kulevya aina ya cocaine hatimaye amekamatwa baada ya kujificha kwa miaka 30 akitumia sura mbalimbali za bandia kukwepa kukamatwa na polisi nchini Brazil.
Da Rocha akiwa na mabadiliko ya sura baada ya operesheni za kubadili muonekano wake
Luiz Carlos da Rocha, ambaye amepewa jina la utani la ‘White Head’ (Kichwa Cheupe), anaaminika kuwa ndiye kiongozi mkuu wa kundi kubwa linalojihusisha na sawa za kulevya Amerika Kusini.
Anaripotiwa kuwa na utajiri wa Dola za Marekani milioni, sawa na Shilingi bilioni 223.9 kutokana na kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya zinazosumbua sehemu za bara hilo la Amerika Kusini.
Da Rocha alipokuwa akiingia kwenye gari la polisi baada ya kukamatwa
Polisi nchini Brazil wamesema kuwa da Rocha alikamatwa Jumamosi jijini Sorisso katika jimbo la Mato Grosso.
Da Rocha alibadili jina lake na kuwa Vitor Luiz de Moraes akiwa na sura ya bandia ili kuficha sura yake, lakini polisi wakafananishe picha zake za zamani na muonekano wake wa sasa na kujiridhisha kuwa waliyemkamata ni mtu sahihi.
Msako wa kumkamata, uliopachikwa jina la – Operation Spectrum – ulishuhudia wanausalama 150 wakipambana na makundi hayo ya kihalifu zaidi ya mara ishirini ambapo walifanikiwa kukamata na kutaifisha magari ya kifahari yenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 10 (sawa na shilingi bilioni 22.4), ndege na mashamba.
Polisi wanasema kuwa kundi lake limekuwa likijihusisha na biashara ya dawa za kulevya nchini Peru, Colombia na Bolivia, na kuzisafirisha kwenda nchini za Ulaya na Marekani kupitia Brazil na Paraguay.
Polisi wanakadiria kuwa da Rocha ana mtandao mkubwa ambao huwa unaingiza dawa za kulevya aina ya cocaine zipatazo tani 5 kwa mwezi nchini Brazil peke yake.
Da Rocha aliweza kukwepa polisi kwa miaka 30 kwa kujibadilisha muonekano Picha: EPA/Polisi Brazil
Polisi pia inamtuhumu da Rocha kuwa ni mmoja wa wasambazaji wakubwa wa dawa hizo za kulevya kwa magenge yanayojihusisha na biashara hiyo pamoja na vitendo vya uhalifu katika majiji ya Sao Paulo na Rio de Janeiro.
Polisi wanamuelezea da Rocha kuwa ni “mhalifu aliyeishi kwa siri sana na kwa tahadhari ya hali ya juu kwa miaka yote hiyo.” Da Rocha anasifika kwa uhalifu ambapo kundi lake limekuwa likitumia silaha za moto na magari yasiyoingia risasi.
Da Rocha anakabiliwa na kifungo cha zaidi ya miaka 50 gerezani kwa tuhuma za kusambaza dawa za kulevya nchi za nje na kutakatisha fedha zilizotokana na biashara haramu.
Masanduku yaliyojaa pesa, bastola na vitu vyengine vya da Rocha Picha: EPA/Polisi Brazil
Polisi wanategemea kuwa sasa wanaweza kukamata na kutaifisha mali zake zote ambazo baadhi yake zinaaminika kuwa ni pesa zilizohifadhiwa katika benki za nje ya nchi.
Da Rocha alikamatwa sambamba na msaidizi wake.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post