KIUNGO WA UKWELI, MCONGO AMESHATUA DAR KUMALIZANA NA YANGA

Kiungo wa Mbambane Swallows aliyekuwa akisakwa kwa nguvu kubwa na Klabu ya Yanga, Kabamba Tshishimbi ametua jijini Dar kwa ajili ya kumalizana na klabu hiyo ya Jawangani.
Kabamba ambaye ni raia wa DRC Congo anayekipiga katika Klabu ya Mbambane Swallows ya Swaziland, ameshafanya mazungumzo na inaelezwa kuwa muda wowote kuanzia sasa anaweza kusaini mkataba wa miaka miwili.
Hivi karibuni, Kabamba aliwahi kunukuliwa akisema kuwa endapo dili hilo litakamilika kwake atakuwa hajakosea ambapo amefuatilia taarifa zake na kuona siyo timu inayokosa mafanikio kutokana na kushiriki mara kwa mara mechi za mashindano ya Afrika.
Kwa muda mrefu Yanga wamekuwa wakisaka mchezaji mwenye uwezo wa Kabamba, atakayeweza kukaba na kuzuia mashambulizi ya timu pinzani walifanya hivyo kwa Justine Zullu, lakini kiungo huyo alishindwa kufanya vizuri.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post