KIUNGO WA ZAMANI WA YANGA ATUA MTIBWA SUGAR

Kiungo Hassan Dilunga amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Mtibwa Sugar ya Turiani, Manungu mkoani Morogoro. 
Hassan Dilunga ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga, ametua klabuni hapo akitokea JKT Ruvu iliyoshuka daraja msimu uliopita, ni kati ya wachezaji wawili waliosajiliwa na Mtibwa Sugar mwishoni mwa wiki, mwingine ni mshambuliaji Riffat Hamisi Msuya kutoka Ndanda FC ya Mtwara.
Wawili hao wanafanya idadi ya wachezaji wapya waliosajiliwa Mtibwa Sugar kufika sita, baada ya awali mabingwa hao mara wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, 1999 na 2000 kuwasajili kipa Shaaban Kado kutoka Mwadui, mabeki Hussein Idd kutoka Oljoro JKT, Salum Kupela Kanoni kutoka Mwadui na kiungo Suleiman Kihimb ‘Chuji’ kutoka Police Moro.
Mtibwa yenyewe imeshawapoteza kipa Said Mohammed, mabeki Ally Shomary na Salim Mbonde waliohamia Simba.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post