KUSOMA VITABU KUNAVYOHUSISHWA NA MAFANIKIO MAKUBWA KIMAISHA

Baadhi ya watu wenye mafanikio makubwa zaidi kwenye nyanja mbalimbali wana tabia moja: si kwamba wana akili nyingi sana, wala si kwamba bahati ya mtende iliwadondokea, ila ni kwa wao kuthamini sana na kuwa na tabia ya kupenda kusoma. Vitabu ndio vimekuwa mtaji uliowapa mafanikio makubwa, kabla na hata baada ya kuwa na mafanikio makubwa kifedha.
Kuanzia mtaji wa dola 2 za Marekani (Tsh. 4,600) mpaka kufikia dola bilioni 20 (trilioni 4.6), vijana wawili walipata kazi katika mgahawa mjini Omaha, Nebraska. Mkubwa katika vijana hao ambaye alitoka katika familia maskini iliyoathiriwa kutokana na mtikisiko wa kiuchumi wa dunia, alikuwa akitengeneza mapochi na kuyauza ili kuweza kumudu maisha. Kijana mdogo kati yao, ambaye alikuwa ni mjukuu wa mgahawa huo ambao walighairisha kwenda chuo kikuu na kuamua kufanya kazi za hapa na pale kama kuuza ‘big g’ na kuuza soda za Coca-Cola majumbani mwa watu.
Kipindi hicho, kila mmoja alikuwa akipata kiasi cha dola za Marekani 2 kwa siku. Miaka kadhaa tu baadaye, wakaingia kwenye kundi la watu wanaoingiza faida ya dola za Marekani bilioni 20 kwa mwaka katika biashara mbalimbali wanazofanya maeneo ya Berkshire Hathaway. Wavulana hawa ni akina nani? Si wengine zaidi ya Charlie Munger na mwenzake Warren Buffett.
Ilikuwaje wakawa wawekezaji wenye mafanikio zaidi katika historia ya Marekani?
Buffett anatumia asilimia 80% ya siku yake kusoma, na rafiki yake ambaye sasa ana umri wa miaka 84, Charlie Munger, alisema kwenye kundi la wanafunzi wa Sheria kwamba siri kubwa katika mafanikio waliyoyapata ni:
“Mara nyingi tu nawaona na watu wakifanikiwa maishani bila wao kuwa watu wenye akili nyingi zaidi ya wengine, na mara nyingine hata sio kwamba wanafanya kazi sana kuzidi wengine, bali wamekuwa wanajifunza kwa kasi kama mashine. Kila siku wanapanda kitandani wakiwa na ufahamu mkubwa zaidi ya waliokuwa nao walipoamka asubuhi na ndugu zangu, hilo linasaidia sana, hasa kama una ndoto za kufika mbali maishani mwako.”
Kwa mfano, katika siku za mwanzo za Buffett katika kujihusisha na uwekezaji, ungemkuta anasoma kurasa kati ya 600 hadi 1000 kwa siku moja.  Siku hizi, bado anatenga asilimia 80 ya siku yake akiwa anasoma vitabu.
Ushauri wake kwa kila mmoja: bila kujali upo chini kiasi gani kimaisha, endelea kujifunza na mafanikio yatakuja tu.
Klabu ya kusoma ya mabilionea
Si mabilionea Buffett na rafiki yake Munger pekee wanaohusisha mafanikio yao kimaisha na tabia yao ya usomaji.
Mfanyabiashara katika sekta ya teknolojia, Elon Musk mara nyingi amesema kuwa alijifunza jinsi ya kutengeneza roketi kwa kusoma vitabu. Musk alikuwa akinyanyaswa sana na watoto wenzake utotoni nchini Afrika Kusini. Faraja pekee akawa anaipata kwenye vitabu vya hadithi za kubuni na vitabu vya kubuni vya kisayansi, vitabu ambavyo vilimhamasisha kufanya kitu kitakachoacha historia duniani.
Bill Gates, mtu tajiri zaidi duniani kwa sasa na miongoni mwa watu wanaosema zaidi vitabu aliwahi kusema kuwa anasoma vitabu visivyopungua 50 kila mwaka, lakini hasomi kabisa vitabu vya kubuni. Ingawa anapata fursa ya kutembelea sehemu nyingi na kukutana na watu wenye uelewa mkubwa, anasema anaona ni bora zaidi kusoma vitabu ili kujiongezea maarifa zaidi.
Hivyo hivyo, bilionea kijana na mmiliki wa mtandao wa Facebook, Mark Zuckerberg mnamo mwaka 2015 alialika watu wote duniani waungane naye katika kampeni yake ya kusoma kitabu kimoja kila wiki.
Je, malengo yako ya kusoma ni yapi?
Unahitaji kwenda kulala ukiwa na ufahamu mkubwa zaidi?
Ingawa kusoma kuna thamani kubwa sana, watu wengi wanaichukulia kama kazi ngumu sana kuifanya. Kwanini usome kama unaweza kumalizia siku yako kwa kipindi cha runinga unachokipenda zaidi? Au kukaa na marafiki zako wapendwa? Wakatu unajiuliza maswali haya ambayo yawezekana kuwa ni ya msingi sana kwako, kumbuka pia kujiuliza nini unachokosa kama ungejijengea tabia ya kusoma na baadae maishani kuwa na mafanikio ya japo robo tu ya Bill Gates, Warren Buffet au Mark Zuckerberg?
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post