KWA HALI ALIYO NAYO… DUA ZENU KWA MZEE MAJUTO

Mzee Majuto.

MKE WA MZEE MAJUTO AFUNGUKA
Baada ya kupata habari hizo, Amani lilimtafuta msanii huyo kwa njia ya simu yake ya kiganjani ambapo ilipokelewa na mkewe, Aisha Yusuf ambaye alithibitisha mumewe kuumwa.

Mama Majuto alisema kuwa, hadi wakati anazungumza na gazeti hili alikuwa yupo na mumewe katika Hospitali ya Tanga Central Health Centre (TCHC) ambako alilazwa kwa siku tano na kufanyiwa upasuaji.
“Ni kweli Mzee Majuto anaumwa ndiyo maana nimepokea simu yake, nipo naye hapa hospitalini, anasumbuliwa na ugonjwa wa hernia ambao umeibuka na kumuanza tena.
“Tunamshukuru Mungu kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji hivyo Watanzania na mashabiki wake waendelee kumuombea na Mungu akipenda hivi karibuni tu atarudi mzigoni, watarajie mambo mazuri kutoka kwake,” alisema mama Majuto.

Amani lilipoomba kuzungumza na Mzee Majuto mwenyewe, mkewe alisema alikuwa usingizini kwani alitakiwa apumzike baada ya upasuaji.
“Nitamfikishia pole lakini haruhusiwi kuzungumza, anatakiwa kupumzika,” alisema mama huyo na kuongeza:
“Hata hivyo, tumeambiwa tutaruhusiwa kutoka hapa hospitalini muda wowote.”

MASHABIKI WAMMISS
Wakiongea na gazeti hili, baadhi ya mashabiki wa staa huyo walisema kuwa, wamemmiss sana kwenye fani yake ya uigizaji na kumuomba Mungu afanye miujiza na amrejeshee afya yake.
“Kwa kweli tumemmiss sana, tunaamini atapona na kurejea kwenye hali yake ya kawaida,” alisema mmoja wa mashabiki aliyejitambulisha kwa jina la Said Juma.
UGONJWA WA HERNIA
Hernia au ngiri ni aina ya ugonjwa ambao humpata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikilia au kubeba viungo (organs) fulani kupoteza uimara au kuwa na uwazi (opening) hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiliwa ipasavyo.

Miongoni mwa vitu vinavyoweza kumsababisha mtu kupata hernia ni pamoja na kuwa na uzito mkubwa au kuongezeka uzito kwa ghafla, kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu, ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua.
Pia kuharisha au kuvimbiwa (constipation). Vitu hivyo humfanya mtu apate hernia ambayo husababisha afanyiwe upasuaji ili kumaliza tatizo hilo.

Stori: GLADNESS MALLYA, DAR
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post