KWA NINI WENGINE HUTOKWA JASHO ZAIDI, NA NINI CHA KUFANYA?

SHARE:

Watu wote huwa wanakuwa na idadi karibu sawa za vinyweleo vya kutolea jasho, lakini vifuko vya kutoa jasho huwa vinakomaa miaka miwili ya...

Watu wote huwa wanakuwa na idadi karibu sawa za vinyweleo vya kutolea jasho, lakini vifuko vya kutoa jasho huwa vinakomaa miaka miwili ya mwanzo wa maisha. Si vifuko vyote vya jasho vinakuwa na uwezo wa kutengeneza jasho (inategemea mahitaji ya mwili kwa muda huo). Watu wanaoishi kwenye hali ya hewa ya joto huwa wanakuwa na vifuko vinavyofanya kazi zaidi ya waliokua kwenye hali ya hewa ya baridi. Kwa watu wazima, tunakuwa na vifuko vyote lakini ni asilimia ndogo tu ndio vinavyotengeneza jasho.
Hali ya hutokwa jasho zaidi ya wengine (ambayo kitaalamu hujulikana kama hyperhidrosis) ni ya kwawaida ingawa yawezekana ikawa inakusababishia aibu mbele ya wengine. Taarifa kutoka jarida la ‘The Science of Us’ zinaeleza kuwa hakuna sababu za kibaiolojia juu ya hali hii.
Kuna mambo kadhaa yanayousababisha mwili kutoka jasho:
1. Mwili unaanza kutoa jasho hata kabla ya joto kuwa kali sana. Lengo kubwa la mwili kutoa jasho ni kulinda joto la mwili. Kwahiyo, mwili huwa unapokea mabadiliko haraka sana hata kama mabadiliko hayo yakiwa ni madogo katika joto la hali ya hewa. Jasho linaanza kutoka hata kabla hatuaanza kupata kero za joto kali, kwahiyo lile jasho linalokutoka kabla ya hali ya hewa kuwa na joto kali si jambo la kushangaza ila ni jinsi mwili unavyotakiwa kufnaya kazi.
2. Kutokwa jasho kunasababishwa na hali ambazo huwezi kuzitawala, na hali hii imetengenezwa na mwili wako ukiwa mtoto. Hii inamaanisha kuwa kutokwa jasho sana haihusiani na tatizo la kurithi hali hiyo. Kwa hiyo hii inamaanisha kuwa mazingira uliyokuwa ukiishi utotoni mwako ni jambo kubwa sana litalofanya uwe unatokwa jasho kwa kiasi gani katika maisha yako ya baadae.
3. Mwili wako kutoa jasho husaidia vidonda kupona. Vifuko vya jasho vinavyojulikana kwa jina la kitaalamu la “eccrine” ambavyo vinakuwepo kwenye mwili mzima ni muhimu sana kwa kufanya vidonda vikauke haraka. Husaidia sana utengenezwaji wa seli mpya mwilini na kuzitoa zilizokufa kutokana na majeraha ya vidonda. Hii inamaanisha kuwa, vifuko vya jasho ambavyo havitapata nafasi ya kufanya kazi utotoni mwako vitarudisha nyuma uwezo huu mwilini mwako — vifuko vya jasho huwa vinachangia uponyaji wa vidonda mwilini kwa asilimia 100 kwa vijana, lakini uwezo huu hupungua kadri umri unavyoongezeka.
Jinsi ya kupunguza kiasi cha kutokwa jasho jingi mwilini:
1. Unaweza kupunguza kutokwa jasho sana kwa kupunguza muda wa kutumia kiyoyozi. Kama huwa muda mwingi unakuwa kwenye joto la chini (baridi), ni rahisi sana kutokwa jasho pindi joto litakapoongezeka, hata kama ni kwa kiwango kidogo sana.
2. Jiweke kwenye mazingira ya joto kubwa mara kwa mara. Kwa kuongeza kiwango cha joto mara kwa mara (hata kwenye gari yako) mwanzoni itakuletea shida ya kutokwa jasho jingi, lakini baada ya muda mwili wako utazoea hali ya hewa ya joto kali. Kama ukijiweka kwenye joto la juu kwa muda, mwili wako utaizoea hali hiyo.
3. Kunywa maji baridi badala ya kujiwekea barafu kwenye sehemu moja tu ya mwili. Uwezo wa mwili kutoa jasho unategemea joto la ndani ya mwili, sio la nje ya mwili, kwahiyo kunywa maji baridi inasaidia kupoza joto la ndani ya mwili—ambalo kwa kufanya hivyo itasaidia kukuweka sawa bila kujali ugumu wa kazi unayofanay au kiwango cha joto cha hali ya hewa, mwili wako bado utapoa kwa haraka.
Utaratibu huu wa kuufanya mwili kuzoea mabadiliko taratibu pia unatakiwa utumiwe unapoanza kufnaya mazoezi. Kana huwa unatokwa jasho hata unapopanda ngazi chache, hata kama hujachoka, endelea tu kupanda nda ngazi—baada ya muda, yawezekana kwa kupanda ngazi hizo kila siku—mwili wako utazoea na utaweza kupanda ngazi hizo hizo bila kutokwa jasho kwa kiwango ambacho kilikuwa kinatoka mwanzoni mwa zoezi hilo.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: KWA NINI WENGINE HUTOKWA JASHO ZAIDI, NA NINI CHA KUFANYA?
KWA NINI WENGINE HUTOKWA JASHO ZAIDI, NA NINI CHA KUFANYA?
https://2.bp.blogspot.com/-_qUu1VL5jHY/WWeK3rEKBoI/AAAAAAAAcxg/1vOJNG20q94WUZFIDq3yL7_1WRWDS2DVgCLcBGAs/s1600/xsweat-1300x500-750x375.jpg.pagespeed.ic.q95oQoPWkz.webp
https://2.bp.blogspot.com/-_qUu1VL5jHY/WWeK3rEKBoI/AAAAAAAAcxg/1vOJNG20q94WUZFIDq3yL7_1WRWDS2DVgCLcBGAs/s72-c/xsweat-1300x500-750x375.jpg.pagespeed.ic.q95oQoPWkz.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/07/kwa-nini-wengine-hutokwa-jasho-zaidi-na.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/07/kwa-nini-wengine-hutokwa-jasho-zaidi-na.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy