LULU AINGIA MKATABA NA JAGUAR

Msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbas `Lulu Diva’.
MSANII wa Bongo Fleva, Lulu Abbas `Lulu Diva’ amejikuta kwenye furaha ya aina yake baada ya kuingia mkataba na msanii kutoka nchini Kenya,Jaguar atakayekuwa anasimamia kazi zake.
Akipiga stori na Showbiz Xtra,Lulu alisema ni jambo la kujivunia kupata shavu kama hilo kwani hakutegemea kama angeweza kupiga hatua kimuziki na kazi zake kusimamiwa na mtu kama huyo mwenye heshima kubwa kwenye gemu ya muziki.
“Namshukuru Mungu kwa hili, nimepata mkataba mnono kwa Jaguar, makazi yangu yataendelea kuwa Bongo, lakini inapotokea nikahitajika Kenya nitakuwa nafika kwa wakati, niwaombe mashabiki wangu waendelee kunisapoti, naamini nitafika mbali zaidi na kuiwakilisha vyema nchi yangu,” alisema huku akigoma kufafanua ni mkataba wa muda gani
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post