LWANDAMINA AMBADILISHIA MBINU AJIBU

Mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu.
KOCHA Mkuu wa Yanga, George Lwandamina anatarajia kuanza program ya uwanjani, leo Jumatatu maalumu kwa wachezaji wake wapya kushika mfumo na mbinu anazozitumia za uchezaji.
Timu hiyo imefanya usajili mdogo kwa kuziboresha baadhi za nafasi ikiwemo ya ushambuliaji ambayo imemsajili, Ibrahim Ajibu kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Simba akiwa mchezaji uhuru.
Yanga itaanza mazoezi hayo ya uwanjani asubuhi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza program ya gym waliyoifanya kwa wiki mbili, ambapo wachezaji hao wapya akiwemo Ajibu watapata nafasi ya kujua mbinu mbalimbali za Lwandamina tofauti na zile walizokuwa wakizitumia walipokuwa kabla ya kutua Yanga.
Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Meneja Mkuu wa Yanga, Hafidh Saleh alisema timu hiyo itaanza mazoezi ya uwanjani baada ya wachezaji kutengeneza fiziki ya kutosha gym.
Saleh alisema, program ya mazoezi ya uwanjani muhimu kwa wachezaji ambao bado hawajaijua falsafa (philosophy) ya kocha ambayo anaitumia, hivyo ni vema wakaanza mapema washike na wazoee.
“Kila mchezaji akitoka kwenye timu moja na kwenda kwingine ni lazima apate ugumu wa kuzoea ‘philosophy’ ya kocha mpya atakayekutana naye.
“Kama unavyojua kila kocha ana mfumo na aina ya uchezaji ya soka la pasi la haraka au taratibu, hivyo basi kocha amepanga kuanza nao kesho (leo) kwa kuwapa mazoezi ya uwanjani.
“Ninaamini kabisa kwa wiki hizi mbili ambazo timu ilikuwa gym ikifanya mazoezi ya gym kwa ajili ya kuongeza fiziki, wachezaji watakuwa fiti tayari na kuanza program ya mazoezi ya uwanjani kucheza mpira ili miili yao ifunguke,” alisema Saleh.
(Stori: Wilbert Molandi | Championi)
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post