MADHARA YA KUTUMIA PAMBA ZA KUSAFISHA MASIKIONI

Damali Namubiru (25) kila mara hutumia pamba za masikioni (cotton swabs/ear bud) kuondoa kile anachodhani kuwa ni uchafu masikioni mwake na baada ya hapo hujisikia mwenye afadhali.
Lakini, baada ya kutumia pamba hizo kuwa tabia yake ndani ya muda mfupi, alisikia hali isiyokuwa ya kawaida ndani ya masikikio yake na hivyo kulazimika kwenda kumuona mtaalamu ili aweze kupatiwa ushauri pamoja na matibabu.
“Nilihisi kama uwezo wangu wa kusikia unaanza kupotea. Nilikuwa nikisia mngurumo ndani ya msikio yangu kwa muda, hivyo inabidi kwenda kumuona mtaalamu ambaye baada ya kunifanyia uchunguzi alinionya kuhusu matumizi ya pamba za masikioni,”  alisema Damila.
Dr. Fred Biso toka nchini Uganda ametahadharisha juu ya matumizi ya pamba hizo kusafisha akisema kuwa kinachodaiwa kuwa ni uchafu (ear wax) ni muhimu kwa afya ya masikio.
Dr Biso alisema kwamba nta ya masikioni ni muhimu kwani hulinda sikio na kusaidia katika mfumo wake wa kujisafisha lakini pia kulilinda dhidi ya bakteria, fangasi, uchafu, wadudu na maji.
Ukosefu wa nta hiyo ndani ya sikio hupelekea sikio kuwa kavu hali inayoweza kukusababishia maumivu, alisema dakatari huyo.
Mtaalamu huyo alionya kuwa masikio yana mfumo wake tofauti wa kufanya usafi na hivyo mtu yeyote hatakiwa kuingilia  mfumo huo.
Dr. Richard Asaba kutoka Hospitali ya Rufaa ya Hoima alisema, katika mchakato wa kusafisha masikio, ngozi laini iliyopo ndani ya sikio inakuwa hatarini kukumbwa na mashambulizi.
Kwa upande wake Dr. Sabrina Kitaka kutoka Hospitali ya Mulago alisema kuwa, kutumia pamba za masikioni kwa muda mrefu ni hatari kutokana na kuathiri ngoma ya sikio.
“Hakuna mtu anayetakiwa kuweka kitu chochote ndani ya sikio akisema anataka kuondoa uchafu. Unaweza kusafisha sehemu ya nje ya sikio kwa kutumia maji na pamba,” alisema Daktari huyo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post