MAGUFULI AWAFUNGA MIDOMO WALIOPINGA MRADI WA UMEME RUFIJI

SHARE:

Rais Dkt John Pombe Magufuli amewahakikishia watanzania kuwa serikali ina fedha za kutosha kujenga mradi wa kufua umeme wa maji, Stiglers...

Rais Dkt John Pombe Magufuli amewahakikishia watanzania kuwa serikali ina fedha za kutosha kujenga mradi wa kufua umeme wa maji, Stiglers Gorge katika Mto Rufiji.
Licha ya kuwa kumekuwepo na baadhi ya watu wakisema kuwa mradi huo utapelekea uharibifu wa mazingira katika Hifadhi ya Akiba ya Selous, Rais Magufuli alisema mradi huo ni lazima ujengwa na tena utasaidia zaidi kuhifadhi mazingira ya eneo hilo.
Liwake jua, inyeshe mvua ni lazima mradi wa Stiglers Gorge ujengwe kwa sababu mbuga ni ya watanzania, eneo ni la watanzania na umeme ni wa watanzania. Kwanza ukiangalia eneo litakalotumika kujenga mradi huo wa umeme ni asilimia 3 tu ya eneo lote la hifadhi hiyo, alisema Rais Magufuli.
Rais ameyasema hayo leo alipokuwa akifungua maonyesho ya 41 ya Sabasaba jijini Dar es Salaam ambapo amesema, kwa watu ambao wamesoma wataelewa kuwa, ujenzi wa mradi huo utasaidia zaidi kuhifadhi mazingira na kuwanufaisha wakazi wa Rufiji kwa kuendesha kilimo pamoja na uvuvi wa samaki.
Uamuzi huu wa Rais Dkt Magufuli umekuja ikiwa ni siku moja tu baada ya kauli ya Wizara ya Maliasili na utalii ambapo imewataka wadau wa uhifadhi kote nchini kuunga mkono mpango wa Serikali wa kujenga mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme katika mto Rufiji kwenye pori la akiba la Selous ambao ukikamilika unatarajiwa kuzalisha zaidi ya megawati 2,100.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudance Milanzi amesema utekelezaji wa mradi huo wa umeme ni wa muhimu kwa taifa kwani utasaidia kuharakisha maendeleo ya taifa kuelekea azima yake ya Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati.
Akiongea wakati akifunga mafunzo ya askari wa wanyamapaori kutoka Mamlaka ya wanayamapori Tanzania -TAWA na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Katibu mkuu Meja Jenerali Gudance Milanzi amesema mradi huo wa umeme pamoja na mradi wa bwawa la maji la Kidunda utachukua eneo dogo tu la pori la akiba la Selou lenye ukubwa wa zaidi ya kilomita za mraba elfu 50.
Amesema pori hilo ndilo kubwa miongoni mwa mapori ya aina hiyo ulimwenguni na ukubwa wake ni zaidi ya nchi za Rwanda na Burundi zikiunganishwa kwa pamoja.
Katibu Mkuu amesema ujenzi wa miradi hiyo hauna tafsiri kwamba Tanzania haithamini masuala ya uhifadhi bali unazingatia uhifadhi wenye manufaa kwa jamii na maendeleo ya taifa na hasa dhamira ya serikali ya rais Dk John Pombe Magufuli kuelekea Tanzania ya viwanda ambayo inahitaji nishati ya umeme itakayoyotosheleza mahitaji ya taifa.
Amesema Tanzania inatambua umuhimu wa uhifadhi ndiyo maana imetenga eneo la zaidi ya asilimia 28 ya eneo lote la nchi kavu Tanzania bara kwaajili ya uhifadhi wa aina mbalimbali ukiwemo wa wanayamapori na misitu ya vyanzo vya maji ambayo ni muhimu kwa shughuli za kijamii na kiuchumi, “ ni nchi chache sana duniani zenye eneo kubwa la uhifadhi kama Tanzania” alisisitiza katibu mkuu.
Katibu mkuu amewataka wafanyakazi wa wizara na watanzania kwa ujumla kutokuwa kikwazo kwa utekelezaji wa mradi huo na kwamba wadau wanaotaka kuisaidia Tanzania wasaidie kuhakikisha inatumia maliasili zake kupiga hatua ya kimaendeleo ikiwemo misaada ya teknolojia za kisasa na rafiki wa mazingira kusaidia kufikia malengo yake kimaendeleo.
“Mtakumbuka mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli hivi karibuni alipokuwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Pwani amezungumzia kwa kirefu sana umuhimu wa miradi hiyo ukiwemo wa bwawa la Kidunda na wa umeme wa Stieglars Gorge, sasa sisi kama wahifadhi na kama watumishi lazima tumuunge mkono na tusiwe kikwazo katika dhamira hii njema” alisema Jenerali Milanzi’’.
Ametoa mfano wa nchi ya Qatar ambayo amesema ilikuwa na eneo la uhifadhi lililokuwa kwenye orodha ya maeneo ya urithi wa dunia kutokana na uwepo wa baadhi ya viumbe adimu lakini walipogundua mafuta, waliamua kujitoa kwenye urithi wa dunia ili wachimbe mafuta na kuinufaisha nchi hiyo na maendeleo ya wananchi wake.
Akizungumzia kuhusu tatizo la mifugo kwenye maeneo yaliyohifadhiwa, Katibu mkuu amewataka wahifadhi kuhakikisha wanakabiliana na changamoto hiyo na kusimamia sheria zilizotungwa na Bunge la Jamahuri ya Muungano wa Tanzania ambazo zinakataza mifugo kuingia hifadhini kinyume cha sheria.
Amesema ndiyo maana serikali inatumia fedha nyingi kugharamia mafunzo ya askari wa wanyamapori na wahifadhi ili kuwaongezea ujuzi na weledi wa kulinda maliasili za taifa kwa kuzingatia sheria zilizopo.
Katibu Mkuu Meja Jenerali Gaudance Milanzi amezungumzia pia umuhimu wa kuhakikisha mapori ya uhifadhi yanatumiwa kwa uhifadhi badala ya kutumika kwa mambo mengine ikiwemo kilimo cha bangi na maficho ya majambazi na majangili na amewataka wahifadhi na askari kushirikiana na vyombo vingene vya ulinzi na usalama kuwafichua wahalifu wanaojificha kwenye mapori hayo na kufanya ujangili na uhalifu mwingine.
Mapema katika taarifa yake kwa katibu mkuu, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania -TAWA Martin Loibooki alieleza kuwa mafunzo hayo yamesaidia kuimarisha uhifadhi kwenye mapori mbalimbali ya akiba nchini na maeneo ya uhifadhi wa wanyamapori.
Aliwashukuru wadau mbalimbali wa uhifadhi wa ndani na nje ya nchi wanaofadhili mafunzo hayo na vitendea kazi juhudi ambazo amesema zimeanza kuzaa matunda ikiwemo kuongezeka kwa idadi ya tembo na wanyamapori wengine kwenye mapori mengi nchini.
Mfunzo hayo yaliyowashirikisha askari wa wanyamapori wapatao 98 kutoka Mamlaka ya wanayamapori Tanzania TAWA na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ni mwendelezo wa mafunzo yanayotolewa na Wizara ya Maliasili na utalii kwa askari wa wanyamapori na watumishi wengine wa wizara hiyo katika hatua za kuelekea mfumo wa jeshi usu.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MAGUFULI AWAFUNGA MIDOMO WALIOPINGA MRADI WA UMEME RUFIJI
MAGUFULI AWAFUNGA MIDOMO WALIOPINGA MRADI WA UMEME RUFIJI
https://2.bp.blogspot.com/-NevaCHH8c5c/WVeYZRECasI/AAAAAAAAcks/yoIEPb1hITAR4EIFmjUTz_GWfOSjl7ncgCLcBGAs/s1600/x11-2-702x375.jpg.pagespeed.ic.dgeHZuHUJ4.webp
https://2.bp.blogspot.com/-NevaCHH8c5c/WVeYZRECasI/AAAAAAAAcks/yoIEPb1hITAR4EIFmjUTz_GWfOSjl7ncgCLcBGAs/s72-c/x11-2-702x375.jpg.pagespeed.ic.dgeHZuHUJ4.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/07/magufuli-awafunga-midomo-waliopinga.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/07/magufuli-awafunga-midomo-waliopinga.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy