MAHAKAMA YA KISUTU YAMUACHIA HURU KAMISHNA WA TRA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemuachia huru aliyekuwa a Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Tiagi Masamaki na mwenzake waliokuwa wakishtakiwa na makosa ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya Tsh bilioni 12.7.
Mahamaka imefikia uamuzi huo baada ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) kusema kuwa hana nia ya kuendele na mshtaka hayo.
Mbali na Masamaki washtakiwa wengine waliokuwa wakikabiliwa na kesi hiyo iliyotokana na sakata la makontena 329 ni Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru TRA, Habib Mponezya (45) na Meneja Msimamizi na Ufuatiliaji wa Forodha, Burton Mponezya (51).
Wengine ni, Msimamizi Mkuu Kitengo cha Ushuru wa Forodha ICD Azam, Eliachi Mrema (31), Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Biashara TRA, Hamis Omary (48), Meneja wa Oparesheni za Usalama na Ulinzi ICD, Raymond Adolf Louis (39) na Meneja wa Azam ICD, Ashrafu Khan (59) na Haroun Mpande (28) wa kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta ICT TRA.
Kwa pamoja wanadaiwa kuwa kati ya Juni Mosi na Novemba 17, 2015 walikula njama kwa kuidanganya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu Sh 12.7 bilioni.
Washtakiwa hao, wanadaiwa ku danganya kuwa Makontena 329 yaliyokuwepo katika Bandari Kavu ya Azam (AICD) yalitolewa baada ya kodi zote kufanyika wakati wakijua si kweli.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post