MAKOSA UNAYOFANYA UNAPOLALA NA MPENZI WAKO

Mwanamke mwenye nywele ndefu unashauriwa kuzielekeza kando mbali na sura ya mpenzi wako mkiwa mmelala namna hii. Itamfanya mwenza wako kuwa huru wakati amelala. Funga nywele zako vizuri na uzielekezee kando ili asije kukosa pumzi kwa sababu ya nywele zako na kutokuwa na umakini.
Mwanamke anapokukumbatia, hakikisha unamfanya awe huru. Epuka ‘kumkaba’ kwani akilala vibaya akiwa amekukumbatia ataamka akiwa na maumivu  ya shingo kutokana na mkono wako.
Kama mwanamke anapenda kulala upande wa ukutani, basi muachie nafasi na uepuke kumsogelea sana. Itasaidia kupata usingizi mzuri na kuboresha uhusiano wenu.
Kama ni wapenzi wa wanyama na mnataka naye alale kitandani pamoja nanyi, hakikisheni mnamlaza miguuni mwenu la sivyo atalala sehemu ambayo itasababisha ajali itayomfanya awadhuru kwa kujihami.
Mnapolala na mtoto, mkumbuke kumlaza katikati yenu na muepuke aina za ulalaji ambazo mwisho wake itaonekana kama mpo kwenye mapambano ya karate au mieleka.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post