MAMA SAMIA ATUMA SALAMU BAADA YA KUMSHUHUDIA ROONEY AKICHEZA TAIFA

Mara baada ya kuishuhudia Everton ikipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Gor Mahia, Makamu Raia wa Tanzania, mama Samia Suluhu‏ ameelezea kufurahishwa na mchezo huo ulivyokuwa na kusema kuwa anaamini Watanzania na wengine wote wameburudika.

Everton ilikuwa jijini Dar es Salaam ikiwa pamoja na staa wa timu hiyo, Wayne Rooney kwa ajili ya kucheza mchezo wa kirafiki chini ya udhamini wa Kampuni ya SportPesa. 

Mchezo huo ulichezwa kwenye Uwanja wa Taifa na kushuhudiwa na maelfu ya mashabiki na viongozi mbalimbali wakiwemo marais wa zamani wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete na Ally Hassan Mwinyi.
 
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, mama Samia ameandika: “Mechi ilikuwa nzuri na yenye kutia hamasa naamini pamoja na kuburudika pia tumejifunza.” 

Katika mchezo huo, Rooney alifunga bao la kwanza la timu yake katika dakika ya 35 kwa shuti kali la mbali lililopita juu ya kipa wa Gor Mahia.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post