MANCHESTER UNITED YAICHAPA REAL MADRID KWA PENALTI

Timu ya Manchester United imeifunga Real Madrid kwa mikwaju ya penalti baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 kwa sare ya mabao 1-1.
Dakika ya 45, Anthony Martial alitumia juhudi binafsi na kumtengenezea pande Jesse Lingard ambaye alifunga bao zuri upande wa United wakati Casemiro aliisawazishia Real Madrid kwa njia ya penalti katika dakika ya 69 baada ya mlinzi mpya wa United, Victor Lindelof kumuangusha Theo Hernandez katika eneo la hatari.
Ajabu katika mchezo huo penalti saba kati ya 10 zilizopigwa baada ya dakika 90 hazikuingia wavuni.
Haukuwa usiku mzuri kwa Lindelof ambaye aliendeleza makosa yake na kukosa mkwaju wa penalty pia licha ya awali kusababisha penalti iliyozaa bao la kusawazisha la wapinzani wao hao.
Kwa ushindi huo sasa, United wameshinda michezo yote minne katika ziara nchini Marekani na watakutana na Barcelona katika keshokutwa Jumatano.
Baada ya mchezo huo wa kirafiki uliochezwa usiku wa kuamkia leo Jumatatu, sasa timu hizo zitakutana katika mchezo wa Super Cup mnamo Agosti 8, mwaka huu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post