MANJI ANASHIKILIWA NA POLISI KWA SIKU YA NNE LEO, SABABU YAELEZWA

Jeshi la Polisi linamshikili mfanyabiashara maarufu Yusuf Manji kwa tuhuma za kukutwa na sare za Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika moja ya maghala ya kampuni zake.
Manji ambaye alimewahi pia kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga anashikiliwa na jeshi hilo tangu Julai Mosi mwaka huu ambapo Polisi wamedai kukuta sare za JWTZ katika ghala la Kampuni ya Quality Motors Group.
Pamoja na Manji wengine waliokamatwa naye ni Deogratius Kisinda na Thobias Fwere wote wakikabiliwa na shtaka hilo.
Wakili wa watuhumiwa hao Hudson Ndusyepo, jana alifungua kwa hati ya dharura ya maombi katika Mahakama Kuu ya Tanzania Dar es Salaam akiomba mahakama iingilie suala hilo ili waachiwe huru au wafikishwe mahakamani na washtakiwe kwa mujibu wa sheria.
Ndusyepo amefungua maombi hayo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro na Mkuu wa Upelelezi Kanda ya Dar es Salaam.
Wakili huyo amesema kwa sasa mteja wake, Yusuf Manji anatibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akiwa chini ya ulinzi wa Polisi.
Hii ni mara ya pili ndani ya mwaka huu kwa Manji kufungua maombi hayo mahakama kuu akiomba kufikishwa mahakamani baada ya kushikiliwa kwa muda ambapo mara ya kwanza ilikuwa Machi alipokuwa akishikiliwa na Idara ya Uhamiaji kwa siku kadhaa bila kushtakiwa.
Watuhumiwa hao walikamatwa kwa muda tofauti ambapo Kisinda alikamatwa Juni 30 mwaka huu, na Manji alikamatwa Julai 1 katika jengo la Quality Group.
Watuhumiwa hao wamenyimwa dhamana na Jaji Lugano Mwandambo kwa sababu ambazo hazijafahamika licha ya upande wa utetezi kufuatilia kwa zaidi ya saa 48.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post