MASANJA: NISINGEONDOKA MAREKANI BILA KUWAONA WATOTO WALIOPATA AJALI

Masanja Mkandamizaji akiwa na watoto Sadia na Wilson majeruhi wa Lucky Vincent wanaotibiwa nchini Marekani.

MMOJA  wa wasanii wa vichekesho waliokuwa wakiunda kundi la Orijino Komedi ambaye kwa sasa ni mchungaji, Emmanuel Mgaya a.k.a Masanja Mkandamizaji, amewatembelea watoto Sadia na Wilson  walioko Marekani kwa ajili ya matibabu.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Masanja Mkandamizaji ameposti picha akiwa na watoto hao na kuandika ujumbe ufuatao.

Masanja akiwa na mtoto Sadia

“Mungu amenipa neema ya kwenda kuwaona wadogo zetu waliopata ajali, Sadia na Wilson na kuwepo Marekani kwa matibabu….. Imekuwa siku njema kwetu sote tumefurahi pamoja nao kula nao na kumtafakari Mungu kwa pamoja.

…akiwa na watoto hao, wazazi na ndugu zao.

Lakini pia nimezungumza na wenyeji wao waliofanikisha safari ya wao kuja Marekani!! Hakika Mungu ni mwema wameendelea kuimarika na wanaendelea vizuri!!
Shukrani kwa madaktari na kila aliyetenga muda wake kuwaombea,
wazazi wao wanawasalimu na wanawashukuru kwa ushirikiano na maombi yenu.”

Wote wakifurahi kwa pamoja.

Watoto hao ni miongoni mwa wanafunzi wa shule ya Lucky Vincent walionusurika kifo katika ajali ya gari iliyotokea mkoani Arusha mwezi Mei mwaka huu, ambapo inakadiriwa idadi ya waliopoteza maisha ni 33 ikijumuisha wanafunzi na walimu waliokuwa katika gari hilo.
Pia majeruhi hao wanatarajia kurejea nchini Agosti 18, Ijumaa saa 3 asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kutokana na afya zao kuimarika.
Na Isri Mohamed/GPL
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post