MATUMIZI MABAYA 7 YANAYOFANYA WATU WACHELEWE KUMILIKI NYUMBA ZAO

Asilimia kubwa ya vijana kwa sasa wanashindwa au wanachelewa sana kumiliki nyumba zao wenyew kwa sababu ya kipato kidogo au kuelemewa na mzigo mkubwa wa madeni. jambo linalosababisha pia wachelewe sana kuingia kwenye ndoa na kupata watoto pia na wanajikuta wakipanga kwa muda mrefu sana maishani mwao. Baadhi huwa wanaendelea kuishi na wazazi wao katika umri mkubwa.
Kusubiri muda mrefu mpaka kuja kumiliki nyumba inamaanisha kuwa na muda mrefu wa kujiandaa kifedha kama kumiliki nyumba ni miongoni mwa malengo yako maishani.
Zifuatazo ni njia saba za matumizi mabovu kabisa ya pesa ambazo yakupasa kuziepuka:

1. Kutegemea faida kubwa sana kwa wakati mdogo

Kama mtu anakuuliza ni kwa nini unataka kununua nyumba na jibu lako la kwanza likawa linafanana na  “Kwa sababu natumia pesa nyingi sana kulipa kodi,” au “Kwa sababu ni njia bora ya uwekezaji,” yawezekana kabisa ukawa bado hujajiandaa kiakili kwa majukumu mazito yanayoambatana na umiliki wa nyumba. Mwisho wa siku, kumiliki nyumba sio moja ya mbinu za kujitajirisha.
Kumiliki nyumba kutakutaka siku zote kutumia pesa ili iweze kuwa katika ubora wake ule ule. Itakuwa nafuu zaidi kwako endapo utatafuta nyumba ya bei rahisi na inayokidhi mahitaji yako ambayo si ya kifedha: Iwe kwenye mtaa unaoupenda na ni sehemu nzuri ya kuanzisha familia.
Nyumba haikuingizii faida, sio uwekezaji utakaokulete faida.

2. Kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja

Kuanza jambo kama biashara ni zuri sana, lakini kufanya mambo mengi maishani kwa wakati mmoja yanaweza kukufilisi kwa kasi sana na kukuacha ukiwa huna pesa kabisa.Kwa mfano ukifanya kwa pamoja mambo kama kuoa/kuolewa, kuwa na mtoto, kununua gari na kununua/kujenga nyumba, vyote ndani ya mwaka mmoja, vinaweza vikakufanya uwe hoi bin taaban. Kila moja kati ya hayo linakuja na gharama zake ambazo huwezi kuzitegemea mwanzo wakati unapanga kulitimiza, gharama ambazo zinaweza kukufanya utumie akiba uliyojiwekea kama hujajiandaa.
Kufanya kazi ili utimize malengo ya kifedha uliyojiwekea inachukua muda na inatakiwa ufanye kazi hiyo kulingana na uwezo wako, sio kwa muda ambao unaona ni lazima ufanye jambo hilo au kwakuwa kila mtu unayejuana naye anafanya.

3. Kutumia pesa zako za akiba kufanya malipo ya awali ya nyumba yako

Linapokuja suala la kununua nyumba, unapokuwa na kiasi kikubwa zaidi kwenye akiba yako benki ndio bora zaidi. Lakini pesa unayoitenga kwa ajili ya malipo ya awali ya nyumba — ambayo mara nyingi huwa ni asilimia 20 ya gharama yote — inatakiwa iwe tofauti kabisa na pesa uliyoiweka kwa ajili ya dharura, ambayo huwa ni sawa na gharama yako ya maisha kwa miezi mitatu hadi tisa na ni kwa sababu ya kuweka tahadhari endapo kuna jambo litakwenda tofauti na ulivyotarajia.
Hata kama ukipanga mambo yako vizuri au una mawazo chanya kiasi gani, mara zote kuna mambo ambayo yapo nje ya uwezo wako yatakayokwenda vibaya. Kwahiyo, ni bora kuweka akiba yako sehemu nyingine ambayo ni salama ambayo unaweza kupata pesa hiyo muda wowote, hasa kama unatarajia kuinunua ndani ya miezi mitatu.

4. Kuwekeza pesa yako ya malipo ya awali ya nyumba kwa kununua hisa

Kuwekeza pesa unayotaka kununua nyumba yawezekana ikaonekana ni wazo zuri sana, hasa kama unatarajia kufanikisha lengo hilo kwa muda mfupi. Lakini ukweli ni kwamba hilo si jambo la busara kwako kujaribu kulifanya.
Hakuna kitu kinachouma zaidi ya kutumia pesa ambayo ulitarajia kuifanyia malipo ya awali ya manunuzi ya nyumba kisha soko la hisa liporomoke na kufanya pesa yako ipoteze thamani na kuwa ni pesa kidogo hata ukiamua kuuza hisa zako.

5. Kutokuwa na shughuli ya kipato cha kudumu

Katika maandalizi ya kununua nyumba, hakikisha unakuwa na kipato cha kudumu kwa muda wa angalau kati ya miezi tisa na mwaka mmoja ili uweze kufaulu kupewa mkopo. Mara nyingi unaweza kumsikia mnunuzi wa nyumba akisema, “Nimepata kazi mpya, Nimeanzisha biashara, Nitakuwa mpiga picha, kwahiyo nataka kununua nyumba: na hii inakuwa kama unajimaliza mwenyewe kwakuwa inaonesha kuwa huna kipato kinachothibitisha unastahili kupatiwa mkopo wa nyumba.
Ongea na mtu anayehusika na mikopo walau miezi miwili au mitatu kabla ya kuamua kuhusu ununuzi wako ili ujue ni vipi unaweza kupata pesa, au ujue unatakiwa ufanye kazi kiasi gani kuweza kufaulu kupatiwa mkopo.

6. Kuwa na madeni mengi

Unapoomba mkopo, kiwango cha riba ya kurudisha deni hilo kinategemea kwa kiasi fulani na historia yako ya madeni. Kama bado una madeni, haitakuwa wakati mzuri kwako unapoomba mkopo wa nyumba. Siri kubwa ni upewe mkopo wenye riba ndogo.
Fikiria kitu kimoja: kama utatakiwa kufanya marejesho ya mkopo huu kwa miaka kati ya 15 na 30, utakuja kulipa kiasi kikubwa sana cha riba,. Kwahiyo punguzo dogo tu la riba katika mkopo wako litakuokolea pesa nyingi sana.
Angalia sana madeni yako hasa kwa muda wa miezi sita kabla hujaanza maandalizi ya kununua nyumba. Hili si jambo la kufanya kwa mwezi mmoja tu kwakuwa utakuja kushangaa kuwa una madeni makubwa yatakayokuzuia hata kupewa mkopo mwingine.

7. Kukosea kupiga hesabu za kiasi gani unaweza kukimudu

Kabla hujaanza kuweka bajeti ya kununua vitu vya jikoni au vyumba vingapi unahitaji, ni muhimu sana kujua unahitaji mkopo kiasi gani ambao utaweza kuumudu bila shida.
Pia, ukiacha marejesho unayotakiwa kuyafanya, pia utakuwa na mambo ya kuzingatia kama kodi, bima, bili za maji na umeme,gharama za ukarabati unaotakiwa kufanya, n.k. Gharama zote hizi unatakiwa uziweke kwenye hesabu zako unazotakiwa kuzilipa kwa mwezi.
Kipimo sahihi cha kuweza kumudu mkopo endapo kiwango cha marejesho kwa mwezi kitakuwa ni asilimia 30 au chini ya hapo ya kipato chako cha mwezi kabla ya kulipa kodi, lakini kanuni hii si msahafu. Kama utaweza kufanya marejesho yako kwa mwezi yawe chini ya asilimia 30 ya kipato chako baada ya kukatwa kodi, basi utakuwa na pesa za kutosha za kufanyia mambo mengine.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post