MAWAKILI WA MALINZI NA WENZAKE WAPEWA ONYO KALI

Mawakili wanaowatetea Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi na wenzake wameonywa kutozungumzia kesi hiyo nje ya mahakama kupitia vyombo vya habari.
Onyo hilo limetolewa leo na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri wakati watuhumiwa hao walipofika mahakamani hapo tena, ambapo kwa mara nyingine tena wamekosa dhamana na kurudishwa rumande.
Malinzi na Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa wanakabiliwa na mashitaka mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya ofisi na utakatishaji wa fedha.
Hakimu Wilbard amesema kuwa upande wa utetezi wenyewe wanatambua kuwa mashitaka ya utakatishaji fedha hayana dhamana.
Watuhumiwa hao wamerejeshwa rumande hadi kesi yao itakaposikilizwa kwa mara nyingine Julai 17.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post