MAZUNGUMZO UNAYOTAKIWA KUFANYA NA BOSI WAKO MPYA KABLA YA KUANZA KAZI

Ongea na bosi wako kuhusu majukumu unayotarajiwa kuyafanya pamoja na mshahara wako ili uweze kujua kama itawezekana na bosi wako pia ajue kama atamudu kukulipa kiasi cha fedha unachoomba.
Bosi wako si mtabiri wa kujua kilichomo akilini mwako jambo ambalo ni zuri au kama wangekuwa wana uwezo huo basi angeweza kujua ulivyojisikia ulipopewa kazi ya mwisho.
Lakini kibaya ni kwamba bosi wako hawezi kuanza kuotea tu kuhusu malengo yako ya kitaaluma — ikimaanisha kuwa ni jukumu lako kumwambia kwamba unahitaji upandishwe cheo/mshahara. Hii haimaanishi kuwa mazungumzo haya yatakuwa rahisi kuyafanya lakini ni wa muhimu sana kwa mujibu wa wataalamu wengi.
Wataalamu wa masuala ya utawala wanasema kuwa kuna mambo ambayo unatakiwa kuyazingatia ambayo baadhi yake ni kujali kazi yako, kufanya kazi kwa bidii na pia uongee na bosi wako kuhusu mahitaji au matarajio yako. Hakikisha unawaambia ni kiasi gani cha mshahara unakitarajia na pia unategemea kufikia kwenye cheo kipi pamoja na fursa za kujiendeleza kitaaluma.
Yawezekana wakashindwa kutimiza mahitaji yako yote kwa wakati huo lakini ni jambo zuri sana kama mtakuwa na mazungumzo hayo siku ya kwanza kabisa kwakuwa nao wataweza kukwambia hapo hapo kama wataweza kukulipa au mpango wao katika kutimiza mahitaji yako … je, upo tayari kwa majukumu ambayo unasema unaweza kuyafanya? Na wao pia watakuwa wanakuangalia kwa karibu kuona kama upo tayari kwa majukumu kamubwa au cheo ambacho wataona kinakufaa.
Na pia, unapokuwa kwenye mazungumzo hayo na bosi wako na ukapata fursa ya kumuuliza iwapo unaweza kupata ongezeko la mshahara au marupurupu watazingatia maombi yako kwakuwa wanaona kuwa ni muhimu kwako na wewe ni muhimu kwa maendeleo ya kampuni.
Kwa maneno mengine: Bosi wako bila shaka ana rasilimali za kuweza kukuandaa kwa majukumu makubwa na mapya unayostahili, lakini anahitaji kujua ni nini hasa unachohitaji.
Cha kushangaza ni kwamba ni chini ya nusu ya waajiriwa huwa wanapata msukumo wa kuongea na mabosi wao na hata wakiongea nao, ni wachache zaidi wanakuwa na ujasiri wa kuuliza maswali kuhusu kuongezewa pesa. Lakini kila mmoja alitakiwa aweze kufanya mazungumzo haya.
Bila shaka kama utamwambia bosi wako kwamba unahitaji ongezeko la mshahara au kupandishwa cheo, ni lazima atataka kujua sababu za wewe kudhani kuwa unastahili ongezeko hilo. Hivyo, unatakiwa kujua umeongeza thamani kiasi gani kwenye eneo la kazi, kampuni au kwenye timu yako na mafanikio uliyofikia tangu ulipoongezewa malipo kwa mara ya mwisho.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post