MBUNGE HALIMA MDEE AKAMATWA NA POLISI NYUMBANI KWAKE

Mbunge wa Kawe kwa tiketi ya CHADEMA, Halima Mdee amekamatwa na Jeshi la Polisi leo akiwa nyumbani kwake Makongo Juu jijini Dar es Salaama na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay.
Mdee amekamatwa leo jioni kufuatia amri iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi aliyeagiza Polisi Kinondoni kumkata mbunge huyo kwa tuhuma za kumtukuna Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jioni, Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam Henry Kilewo amethibitisha kukamatwa kwa Mdee ambaye pia ni Mwenyekiti wa BAWACHA.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda amesema kuwa wametimiza agizo la mkuu wa wilaya aliyewataka kufanya hivyo.
Hapi alitoa amri hiyo leo asubuhi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo alidai maneno yaliyotolewa na Mdee yanaweza kupelekea uvunjifu wa amani.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post