MBUNGE WA CCM ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA KWA SIRI

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Alhaj Abdallah Bulembo amechukuwa fomu ya kutetea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Bulembo ambaye pia ni Mbunge wa kiteuliwa na Rais amechukua fomu hiyo kwa usiri mkubwa kwa kile kinachodaiwa kwamba amefanya hivyo kufuatia shinikizo ililokuwa likitolewa na Wazee, viongozi na wanachama wa jumuiya hiyo kumuomba agombee tena nafasi hiyo kwa mara nyingine.
Tofauti na wagombea wengine ambao huchukua fomu zao wakisindikizwa na wapambe pamoja na waandishi wa habari, Bulembo jana mchana alifika katika Ofisi za Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dodoma akiwa katika gari namba T888 DFB aina Toyota Land Cruser lenye vioo vya giza (tinted) akiendesha mwenyewe.
Bulembo alikabidhiwa fomu hizo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dodoma, Gama Juma.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post