MBUNGE WA CCM ATOA MSAADA JIMBONI KWA TUNDU LISSU

SHARE:

MBUNGE wa Singida Magharibi kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Elibariki Kingu amewafuta machozi akinamama wa jimbo jirani la Singi...

MBUNGE wa Singida Magharibi kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Elibariki Kingu amewafuta machozi akinamama wa jimbo jirani la Singida Mashariki linaloongozwa na Tundu Lissu wilayani Ikungi, Singida baada ya kuwanunulia vitanda 52 ili kuboresha huduma za afya kwa mama na mtoto.
Kwa muda mrefu, akinamama hao walikuwa na kilio cha kukosekana kwa huduma hizo, hasa vitanda vya kujifungulia, hivyo kumlilia Kingu aliyeamua kubeba jukumu na mbunge mwenzake.
Akizungumza na TSN Digital kwa njia simu, Kingu alisema ameamua kutoa msaada huo kutokana na maombi aliyoyapata kutoka kwa akinamama wa eneo la Ikungi na pia kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida juu ya kuwasaidia katika sekta ya afya kwa kuwapatia vitanda vya kujifungulia.
“Ni kweli ninatarajia siku yoyote nitakwenda kukabidhi vitanda 86 katika Wilaya ya Ikungi, ambako kuna majimbo ya Singida Magharibi nilipo mimi na jimbo jirani la Singida Mashariki kwa Tundu Lissu, kufuatia maombi ya wananchi hasa akina mama ambao huteseka sana kwa kwenda umbali mrefu kutafuta huduma za afya wakati wa kujifungua,”alisema Kingu.
Kingu alisema kati ya vitanda hivyo 86 vyenye thamani ya Sh. Milioni 48.9, vitanda 52 atavigawa katika jimbo la Singida Mashariki na vingine 34 atavigawa katika jimbo lake la Singida Magharibi.
Amesema kati ya vitanda hivyo 52 atakavyovigawa Singida Mashariki, vitanda 26 ni maalumu kwa ajili ya akinamama kujifungulia na vitanda vingine 26 kwa ajili ya wodi za kawaida. Aidha, amesema katika jimbo lake atakabidhi vitanda 34 vya kujifungulia ambavyo kati ya hivyo, vitanda vinne ni vya kisasa vinavyotumia umeme.
Wilaya ya Ikungi ina jumla ya Kata 28 ambapo kati ya hizo, kata 13 zipo katika jimbo la Singida Mashariki ambapo katika sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 wilaya hiyo ilikuwa na takribani wakazi 272,959.
HabariLeo

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MBUNGE WA CCM ATOA MSAADA JIMBONI KWA TUNDU LISSU
MBUNGE WA CCM ATOA MSAADA JIMBONI KWA TUNDU LISSU
https://1.bp.blogspot.com/-hYXThYpmfgc/WXzgc8pzCRI/AAAAAAAAdLI/qyBhOLMOUbopfTBAMa8qyFymB8o2AushQCLcBGAs/s1600/DBipb52W0AAzoIp.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-hYXThYpmfgc/WXzgc8pzCRI/AAAAAAAAdLI/qyBhOLMOUbopfTBAMa8qyFymB8o2AushQCLcBGAs/s72-c/DBipb52W0AAzoIp.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/07/mbunge-wa-ccm-atoa-msaada-jimboni-kwa.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/07/mbunge-wa-ccm-atoa-msaada-jimboni-kwa.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy