MCHEPUKO AVUNJA NDOA YA JAMES RODRIGUEZ WA BAYERN MUNICH

Kiungo mshambuliaji wa Bayern Munich, James Rodriguez ametengana na mkewe ambaye wamedumu katika ndoa kwa muda wa miaka sita.
Rodriguez, ambaye ametua kikosini hapo hivi karibuni akitokea Real Madrid kwa mkopo, ametalikiana na mkewe huyo, Daniela Ospina, kutokana na kile kilichoelezwa kuwa amekuwa ‘akichepuka’ na mwanamitindo mwingine.
Mrembo ambaye anatajwa kuchangia kuvunjika kwa ndoa hiyo ni Helga Lovekaty ambaye ni mwanamitindo, baada ya mke kugundua akaamua kuchukua maamuzi ya kuondoka nyumbani kwa mchezaji huyo raia wa Colombia.
Wanandoa hao walifunga ndoa wakati Rodriguez alipokuwa na umri wa miaka 19 wakati Ospina alikuwa na umri wa miaka 18. Kwa sasa Rodriguez ana umri wa miaka 26.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post