MESUT OZIL ANATAKA KUBAKI ARSENAL

Kiungo wa Arsenal, Mesut Ozil amekiri kuwa anapenda kusaini mkataba mpya kubaki klabuni hapo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anaingia miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake Emirates na amekuwa kwenye mazungumzo na klabu hiyo kuhusu mkataba mpya.
Inaaminika Gunners wamempa ofa ya ujira wa pauni 250,000 kwa wiki Mjerumani huyo ili abaki, awali alikuwa akilipwa pauni 140,000 lakini alikuwa akitaka kulipwa pauni 350,000.

Akiulizwa na waandishi ziarani Australia ambapo timu hiyo inajiandaa na msimu mpya, Ozil alieleza kuwa bado hajasaini mkataba mpya lakini lengo lake ni kubaki Emirates.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post