MISS GRAND TANZANIA YARUDI TENA

Miss Grand International 2016, Ariska Putri Pertiwi.

BAADA ya kukaa kimya kwa miaka miwili, hatimaye lile shindano kubwa la urembo lijulikanalo kama Miss Grand Tanzania limerudi tena kwa kishindo ambapo safari hii linatarajiwa kufanyika Agosti 11, mwaka huu.

Akizungumza na Showbizmmoja wa waratibu wa shindano hilo, Abrahamu Mahimbo alisema kuwa, kila kitu kinaenda sawa na kwa mara ya kwanza katika historia ya shindano hilo kubwa duniani, wanatarajia kuwa na ugeni mkubwa ukiongozwa na Mshindi wa Miss Grand International 2016, Ariska Putri Pertiwi kutoka Indonesia akiwa na kruu yake.

Ariska Putri Pertiwi.

“Hadi sasa tumepata washiriki 28 ambao tutakuwa nao hadi siku ya fainali Agosti 11 na mshindi atapata tikiketi ya moja kwa moja kuingia katika fainali zitakazofanyika Vietnam kwenye Ukumbi wa Vinpearl Phu Quoc Resort & Villas Convention.

Ariska Putri Pertiwi akishika ngao ya ushindi.

Tunatarajia shindano la safari hii kuwa na mvuto zaidi kutokana na uwepo wa washiriki wenye sifa tunazozitaka so safari hii huenda mshindi wa Tanzania akaibuka na kuwa Miss Grand International huko Vietnam,” alisema Abrahamu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post