MKE WA MWENYEKITI WA KIJIJI AKISIMULIA MUMEWE ALIVYOUAWA USIKU KIBITI

Zaituni Mohamed Mkenda, aliyekuwa Mke wa Mwenyekiti wa Kijiji na Mangwi kilichopo wilayani Kibiti mkoani Pwani amesimulia jinsi wahalifu hao walivyovyamia nyumbani kwake hadi kumuua mumewe.
Mkenda amesema kuwa alikuwa amelala na mumewe,  Hamis Bakari Mkima ndipo watu hao walivamia nyumbani kwake majira ya saa nne na nusu usiku na kuvunja mlango wa chumbani kisha wakaingia ndani.
Mwanamke huyo amesema kuwa watu hao waliokuwa wamejifunika sura zao walimuua mumewe na kuchoma nyumba waliyokuwa wakiishii wakati yeye alipofanikiwa kutoroka.
Waliofariki katika tukio hilo ni Ofisa Mtendaji, Mwarami Shamte aliyekutwa na majereha matatu ya risasi na Mwenyekiti wa Kijiji, Hamis Bakari Mkima aliyekutwa na jeraha moja.
Pia wauaji hao walimpiga, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Londo, Michael Martin risasi ya macho, iliyoharibu macho yake mawili na waliichoma moto nyumba ya yake kisha kutokomea kusikojulikana.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post