MKUU WA WILAYA YA ILEMELA AACHIA NGAZI

Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dk Leonard Masale, ameachia kazi rasmi baada ya kufikisha umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma.
Masale aliyeteuliwa na Rais Dkt Magufuli Juni 26, 2016 amefikisha umri wa miaka 60 ambao kwa mujibu wa sheria anatakiwa kustaafu kwa lazima.
Kiongozi huyo mstaafu amethibitisha kuwa hayupo ofisini kuanzia Julai Mosi mwaka huu na kwamba nafasi yake inakaimiwa na Mkuu wa Wilaya ya Magu, Khadija Nyembo.
Aidha alisema kuwa tayari amepokea mafao yake ya kustaafu kutoka mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma, PSPF, baada ya kuwaandikia barua kuwajulisha kuhusiana na kustaafu kwake miezi sita iliyopita.
Pia Masale amesema kuwa bado anazo nguvu ana anaweza kulitumikia taifa katika nafadi yoyote atakayoteuliwa kuishika.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post