MOURINHO: SINA MPANGO NA BALE KWA SASA

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho.
KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho amese­ma hana mpan­go wa kumsa­jili mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth Bale, kwenye kipindi hiki cha usajili.
Bale amekuwa akitajwa mara kwa mara kuwa anawe­za kujiunga na Manchester United aki­tokea Real Madrid, la­kini Mour­inho am­baye ame­wa hikumfundisha kiungo huyo mshambuliaji amesema hana mpan­go naye kwa sasa.
Mourinho amesema kwa sasa Bale ana fu­raha kwenye kikosi cha Madrid na litakuwa jambo gumu kwake kuondoka kwenye timu hiyo ya Hispania.
Mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth Bale.
Hata hivyo, im­eelezwa kuwa Unit­ed wanaendelea kumwania winga wa Inter Milan, Ivan Perisic, kwa kitita cha pauni mil­ioni 48, zaidi ya shilingi bilioni 136.
United wamekuwa wakitakiwa kutoa kitita cha pauni milioni 100, kama wanamtaka Bale jambo ambalo limekuwa gumu sana kwa United kwa sasa.
Madrid wa­naweza kuwa na wazo la ku­muuza staa huyo kama tu watafanikiwa k u m p a t a staa wa Mo­naco, Kylian Mbappe.
“Sijawahi k u f i k i r i kuhus u B a l e k u o n ­doka Ma­drid kwa sasa, nao­n a kuwa ana fu­raha na anataka kubaki kwenye timu hiyo.
“Ni rahisi kufahamu mchezaji ambaye anawe­za kusajiliwa kwa sasa, lakini siyo Bale, kwa kuwa bado anataka kubaki kwenye timu hiyo.
“Yupo kwenye timu ambayo ina maslahi ma­zuri na inafanya vizuri uwanjani siyo jambo ra­hisi kuondoka hapo,” al­isema Mourinho kocha wa zamani wa Real Ma­drid, Porto, Inter Milan na Chelsea.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post