MTEJA AMUUA SANGOMA BAADA YA KUTOFANIKIWA SHIDA YAKE

Mganga wa jadi, Revocatus Kanjalanga (65) katika Wilaya ya Nkasi mkoani Ruvuma ameuawa kikatili kwa kuchomwa na mkuki mgongoni na mtu asiyefahamika ambaye anadaiwa kuwa ni mteja wake wa muda mrefu.
Ilielezwa kuwa wateja wa mganga huyo walikuwa wakimlalamika kuwa kwa kipindi kirefu mganga huyo amekuwa akiwatibu kwa kuwatoza fedha nyingi za malipo ya matibabu lakini wamekuwa hawaponi kupitia uganga wake.
Mtoto wa mganga huyo aliwaambia waandishi kuwa baba yake aliuawa juzi saa 1:30 asubuhi kwa kupigwa mkuki mgongoni akiwa anatembea mitaani katika kitongoji cha Chawe kilichopo katika Mji wa Namanyere wilayani Nkasi.
Alisema kuwa kwa muda mrefu watu ambao walikuwa wanatibiwa na baba yake walikuwa wakilalamika kutozwa fedha nyingi pamoja na mifugo lakini hawaponi, hali iliyosababisha kuanza kumuona kama tapeli.
Alisema watu hao walikuwa wanalalamikia kutofanikiwa matatizo yao ya kiafya, kutafuta mali pamoja na mazindiko.
“Pengine malalamiko hayo ndiyo yaliyosababisha mtuhumiwa aamue kumuua kwa kumchoma mkuki mgongoni, na aliyefanya hilo hajapatikana na mpaka sasa anatafutwa,” alisema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa anasakwa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post