MUDA MWINGINE KUJUA NINI CHA KUTOFANYA NI MUHIMU ZAIDI YA KUJUA CHA KUFANYA

Bila shaka una orodha yako umeiandika – labda kwenye kitabu cha kumbukumbu, kalenda, kwenye kompyuta au simu yako – orodha ya nini cha kufanya, jambo ambalo ni zuri. Lakini yawezekana kabisa orodha unayoihitaji ni ya nini vya kutofanya
Mfano: kama unajiandaa kwa likizo na unajua kwamba hutakuwa na muda wa kufanya kazi jioni, bila shaka huwezi kuwa unafanya kila kazi inayoletwa mbele yako. Kwahiyo inabidi upange kabla jinsi gani utatumia muda mchache ulionao.
Fanya kazi zitazoleta matokeo makubwa huku ukifikifiria vitu vya kutovifanya
Hili inabidi ulifanye kwa umakini. Bila shaka tayari unajua ni wapi unatakiwa kuelekeza nguvu yako na wapi utapata matokeo ya haraka. Baada ya kujua hili ni vyema ukafanya yanayofanikisha yote mawili kwa wakati mmoja — kuelekeza nguvu na mawazo yako kufanya yatayokuletea matokeo ya haraka hata ukiwa safarini. Chochote nje ya hapo kinatakiwa kuwekwa kwenye orodha ya vitu vya kutofanywa.
Zoezi hili litasaidia kukuonesha ni wapi ambapo umeelekeza nguvu kubwa kufanya vitu ambavyo havina umuhimu mkubwa au kufanya mambo ambayo si lazima uyafanye wewe.
Pia unaweza kuuliza marafiki zako kuhusu “nini cha kuepuka/kutofanya” kupitia mitandao ya kijamii kujua watu wengine wanawaza nini au wanapunguzaje mambo yasiyo na umuhimu kwenye ratiba zao. Baadhi ya majibu yaweza kuwa msaada mkubwa kwako.
Kama upo tayari kuandaa orodha yako ya vitu vya kutofanya, anza kuangalia maeneo haya:
Barua-pepe zisizo za lazima. Kwa kujiondoa kwenye orodha za watu wanaokutumia barua pepe zisizo na maana, kama unapowekwa kwenye kundi kubwa la watu waliotumiwa barua-pepe hiyo bila ulazima wowote wa wewe kuwapo, unaweza kujipunguzia usumbufu mkubwa wa kusoma vitu visivyo na ulazima vinavyokupotezea muda. Uwe na barua-pepe chache ambazo unaweza kuzisoma na kufuta papo hapo ndio jambo zuri zaidi.
Mikutano na vikao visivyokuwa na ulazima. Bila shaka huhitaji kuhudhuria zaidi ya nusu ya mikutano au vikao ulivyoalikwa kwa sasa — hasa ikiwa havina dalili ya kuisha na tayari umeshatoa mchango wako tayari. Ongea na muandaaji na umuombe akutumie ujumbe wa kukuita utakapohitajika (na ajue kwamba kama uwepo wako si lazima, omba uondolewe kwenye orodha hiyo.)
Kutatua matatizo/changamoto. Hili limo kwenye uwezo wako. Amua sasa kwamba hutashtushwa na matatizo madogomadogo au kukurupukia matatizo ambayo yanaweza kutatuliwa na mtu mwingine wenye uwezo wa kuyatatua. Si lazima kila tatizo ulitolee ufumbuzi wewe.
Taarifa za mara kwa mara za maendeleo ya kazi. Huna haja ya kupoteza muda wako kufikiria kuhusu maeneo ambayo tayari yanakwenda vizuri. Kama unataka kujua maendeleo, unaweza kufanya ukaguzi wa jumla kwa kulinganisha ulipo na malengo uliyojiwekea kama vinakaribiana. Jipe nafasi ya kutafuta majibu ya mambo ya muhimu au matatizo ambayo yanakuhitaji wewe na utaalamu wako.
Kujua nini hutakifanya inakusaidia ni wapi utoe msaada na wapi uachie wengine.
Ukishaandaa orodha yako ya vitu vya kutofanya utaona jinsi unavyoweza kupata muda ambao mwanzo ulikuwa unapotea bila sababu. Hii haimaanishi kwamba usiendeelee kuiboresha orodha yako ya vitu vya kufanya, ila sasa unaweza kuweka akili yako kwenye malengo ya muda mrefu zaidi. Pia itakusaidia kujiweka karibu na watu wenye uwezo wa kutatua matatizo na changamoto zinazotokea bila kukutegemea wewe hivyo kukuacha uwe huru zaidi kufanya mambo ya muhimu.
Kwahiyo angalia vizuri kazi zako za kila siku. Amua kipi hutakifanya kabisa ili wafanye wengine. Jipe nafasi kubwa ya kufanya kazi itayoleta matokeo makubwa zaidi na uwape nafasi watu wengine kufanya hivyo hivyo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post