MWANAMKE ALIYEANGUKA NA UNGO DAR APEWA MKONG’OTO

Mwanamke mmoja mkazi wa jijini Dar es salaam ambaye jina lake halikufahamikaa amezua kizaazaa baada ya kuanguka na ungo akiwa uchi wa mnyama. Tukio hilo lililoshuhudiwa na watu kadhaa lilitokea karibu na eneo la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Ukonga Banana.
Mwanamke huyo alianguka katikati ya barabara akiwa kwenye ungo ambao alikuwa ameukalia, na nguo pekee alizokuwa amevaa ni sidiria nyeupe kilemba cheupe alichofunga kichwani.
Video ilisambaa jana kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha mwanamke huyo aliyeanguka katikati ya barabara akiwa amekalia ungo ukiwa na unga ambao mwingine alikuwa amejipaka usoni, na masikioni alikuwa na ‘earphones’ kwa ajili ya kusikiliza jambo.
Mwanamke huyo alionekana kuamka baada ya kugundua kuwa alikuwa yupo katikati ya barabara lakini alipovuka na kwenda kando ya barabara hiyo, alionekana kuokota pochi lake pamoja na gauni jambo lililozua mjadala wa tukio zima. Kwamba gauni pamoja na pochi vilifikaje pale alipoviokota kwakuwa hakuwa navyo wakati anaanguka.
Gumzo limekuwa kubwa kwakuwa watu wanaona tukio lenyewe halitoi picha halisi ya mama huyo huku wengi wakihoji endapo ni moja tu ya mbinu za ‘kutafuta kiki za umaarufu’ kama zilivyozoeleka katika kipindi cha hivi karibuni kwa mtu kuwa tayari kufanya hata jambo la kujidhalilisha ili ajulikane. Lakini kama hili ndio lilikuwa lengo basi yawezekana hakupata matokeo aliyotarajia kwani aliambulia kichapo kikali kutoka kwa wananchi waliomzunguka wakimtuhumu kwa uchawi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post